Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Paul Simon Singi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kisanda amehukumiwa kwenda jela Miaka 3 au kulipa faini ya Tsh. 750,000 kwa makosa ya kuomba rushwa ya Tsh. 800,000 na kughushi nyaraka kinyume cha Sheria.
Alifanya uhalifu huo Mei 22, 2023 kwa lengo la kumhalalishia Fabiano Daudi umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa Ekari 3 katika eneo lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika Halmashauri ya Wilaya Kibondo.
Inaelezwa baada ya kupokea Fedha, alitengeneza nyaraka ya kughushi ikionesha mauziano yenye thamani ya Tsh. 800,000 kwa kutumia jina la Josephat Gwimo (Mwenyekiti wa Kitongoji aliyemaliza muda wake)
Chanzo: TAKUKURU