LGE2024 Kigoma: Polisi kufanya uchunguzi wa tukio la mwenyekiti wa kitongoji cha Muyanga C kukutwa barabarani akiwa hajitambui

LGE2024 Kigoma: Polisi kufanya uchunguzi wa tukio la mwenyekiti wa kitongoji cha Muyanga C kukutwa barabarani akiwa hajitambui

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linafanya uchunguzi wa tukio la Onesmo Simon, miaka 40, askari wa Kampuni binafsi ya ulinzi Kiwango Security na Mwenyekiti wa kitongoji cha Muyaga "C", Kata ya Kitahana, Wilaya ya Kibondo kukutwa akiwa hajitambui amelala kando ya barabara ya Kibondo - Kasulu akiwa na michubuko usoni pamoja na puani.

Kupata taarifa na matukio yote kuhusu uchaguzi serikali za mitaa ingia hapa: LGE2024 - Dar es Salaam: Matukio yaliyojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024

Majeruhi Amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo akiendelea kupatiwa matibabu, upelezi wa tukio hili unaendelea.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linaendelea kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia na kubaini uhalifu na wahalifu kwa lengo la kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Imetolewa na:
Filemon K. Makungu - SACP
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kigoma


Screenshot_20241204_174746_Instagram.jpg


PIA SOMA
- Kigoma: Onesmo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Muyaga(CHADEMA) aokotwa akiwa hajitambui baada ya kutupwa
 
Back
Top Bottom