LGE2024 Kigoma: Polisi wafanya uchunguzi wa tukio la mtu aliyekamatwa na kura feki zilizokuwa zimeshapigwa

LGE2024 Kigoma: Polisi wafanya uchunguzi wa tukio la mtu aliyekamatwa na kura feki zilizokuwa zimeshapigwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Niseme tu kwamba nashangazwa na wingi wa matakamko ya polisi siku mbili hizi, yaani ni bandika bandua!

Screenshot_20241128_210807_Instagram.jpg



PIA SOMA

- LGE2024 - Kigoma: Vijana wawekwa chini ya ulinzi kwa wizi wa kura baada ya polisi kuingilia kati
 
Hivi hua wanachunguza nini, wakati mtu ameshikwa na ngozi?
 
Polisi wa nchi wajengewe ukumbi wawe wanachekesha kwa kiingilio. Tangu lini wakawa na ubavu wa kuiwajibisha ccm.??
 
Mbona jana kura bandia zilitamalaki karibu kila kituo cha kupigia kura?

Mfano, msimamizi kwenye kituo kimojawapo Dar (ambaye ni mwalimu) anasema wapiga kura waliokuja kituoni hapo na kupiga kura hawakufika 20.

Wagombea wote wa hapo walikuwa ccm maana wengine walienguliwa.

Wasimamizi waliletewa mifuko ya karatasi za kura wakaelekezwa kupigia kura hao wa ccm ili masanduku yajae.

Ilipofika jioni wakaambiwa hakuna haja ya kufungua masanduku na kuhesabu kura zilizomo. Walipewa tu karatasi zenye data za kura za uongo ili wajaze kwenye fomu za matokeo kama hivi:-

Jina la mgombea...........
Waliojiandikisha 590
Waliopiga kura 581
Kura halali 572
Kura zilizoharibika 9

Inasikitisha sana sana!!!
 
Back
Top Bottom