Mbona jana kura bandia zilitamalaki karibu kila kituo cha kupigia kura?
Mfano, msimamizi kwenye kituo kimojawapo Dar (ambaye ni mwalimu) anasema wapiga kura waliokuja kituoni hapo na kupiga kura hawakufika 20.
Wagombea wote wa hapo walikuwa ccm maana wengine walienguliwa.
Wasimamizi waliletewa mifuko ya karatasi za kura wakaelekezwa kupigia kura hao wa ccm ili masanduku yajae.
Ilipofika jioni wakaambiwa hakuna haja ya kufungua masanduku na kuhesabu kura zilizomo. Walipewa tu karatasi zenye data za kura za uongo ili wajaze kwenye fomu za matokeo kama hivi:-
Jina la mgombea...........
Waliojiandikisha 590
Waliopiga kura 581
Kura halali 572
Kura zilizoharibika 9
Inasikitisha sana sana!!!