Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Wananchi wa Jimbo la Muhambwe Mkoa wa Kigoma amefurahishwa na maamuzi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 2025 yaliyompitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.
Hayo yamejiri wakati Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Mhe. Dkt. Florence Samizi alipofanya ziara kwenye Kata 8 ikiwemo Kata ya Busunzu, Kizazi, Kagezi, Mkabuye, Kumsenga, Busagara, Rugongwe na Nyaruyoba kwaajili ya kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya zake na kufanya mikutano ya ndani na mikutano ya hadhara ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu
Dkt. Florence Samizi ametumia ziara kuwaeleza Wananchi wa Muhambwe kuwa CCM imemteua Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa Tanzania 2025, Dkt. Emmanuel Nchimbi (Katibu Mkuu CCM) kuwa Mgombea nafasi ya Makamu wa Rais na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa Mgombea Urais Zanzibar, na hivyo wananchi wa Muhambwe hawana budi kuwaunga mkono.
Akitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Muhambwe, Dkt. Samizi alisema kuwa, Wana Muhambwe wote watampa kura Rais Samia Suluhu Hassan kwani Muhambwe (Busagara) imepiga hatua kubwa kimaendeleo kutokana na fedha nyingi zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita kwaajili ya Ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, Vituo vya Afya na Zahanati, Sekta ya Elimu (Chuo cha VETA), Kilimo pamoja na miradi ya Maji.
Aidha, Dkt. Samizi alifanya mikutano ya hadhara katika Kata za Kumsenga na Kizazi ambapo alitoa mifuko 40 ya Saruji kwaajili kusakafia jengo la Zahanati ya Kijiji cha Kasana Kata ya Kizazi kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo.
Muhambwe Tunasema Samia Suluhu Hassan Mitano Tena, Tukutane Kwa Balozi

Attachments
-
WhatsApp Image 2025-03-03 at 15.28.39 (1).jpeg607.4 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2025-03-03 at 15.26.53.jpeg431.2 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2025-03-03 at 15.26.53 (1).jpeg294 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2025-03-03 at 15.33.36.jpeg220.2 KB · Views: 1 -
Screenshot 2025-03-03 at 16-35-38 Dkt. Florence Samizi (@florence.samizi) • Instagram photos a...png814.2 KB · Views: 1 -
Screenshot 2025-03-03 at 16-35-47 Dkt. Florence Samizi (@florence.samizi) • Instagram photos a...png744 KB · Views: 1 -
Screenshot 2025-03-03 at 16-36-11 Dkt. Florence Samizi (@florence.samizi) • Instagram photos a...png820.5 KB · Views: 1