Baada ya kushuhudia vurugu hizo, tumezungumza na baadhi ya wananchi waliokuwa mashuhuda ambapo wamesema ni kutokana na mvutano wa uhasimu wa vyama baina yao kwa kila mmoja kuvutia upande wake kwa kutaka kuona hakuna udanganyifu wowote wa kura unafanyika kituoni.
Wakati zoezi la Uchaguzi wa Serikali za mitaa ukiendelea, vurugu zimeibuka katika Kituo cha Shule ya Msingi Kibirizi, Manispaa ya Kigoma Ujiji, hali iliyopelekea Jeshi la polisi kuingilia kati na kutuliza vurugu hizo.
Unajua huu ndo uchaguzi muhimu mno. Hakuna nyumba isiyo na msingi bora. Determination ya ushindi 2025 ni sasa. Hapa ndo CCM itasema tulishinda 2024 na sasa njia nyeupe. Kumbe ni kutumia tu nyundo na si jembe.