Kigoma Yatengwa! Usafiri balaa ..

Naijua Tanga vizuri sana. Tanga ya miaka 60 na 70 siyo Tanga ya leo imerudi nyuma sana kimaendeleo maana wakuu wameamua kuitelekeza.
Ule wimbo wa Wagosi wa Kaya (Tanga kuna nini)ni mfano mzuri wa maelezo yako...
 
Kamanda, umewakusudia nini wazenj?

Sina nia mbaya na Wazenj ni watu wangu wa karibu ila huwa nasonononeka sana na majibu ya kebehi yanayotolewa kuhusiana na mambo mbali mbali ya kero za Muungano...

Lets carry on...
 
Kwa aina hii ya usafiri wa reli huko India sidhani kama watafanya lolote jipya hapa kwetu.
 

Attachments

Umuhimu wa mkoa wa Kigoma (mkoa wa mpakani) haujulikani kwa serikali mpaka mbunge wa Kigoma aseme? miaka yote hii toka uhuru hakuna mtu serikalini anajua hili?
Tungekuwa makini kujenga daraja la mto Malagalasi tungeweza kushindana na Kenya kuwin biashara na Nchi za Maziwa Makuu. Isaka, bandari ya nchi kavu, ilitegemewa sana kuunganisha mizigo kwenda nchi hizo; nayo pia imedoda. Hakuna nchi ya Maziwa makuu yenye hamu ya kupitisha mzigo wake Tanzania kutokana na miundombinu mibovu inayoelekea mji wa Kigoma. Tulipaswa kuliona hili mapema,lakini hatujachelewa kufuatia vurugu za Kenya (eenh, waswahili usema kufa kufaana)!

Jana Waziri wa Biashara wa Rwanda ameongea kusudio la nchi yake kuwa partner ktk business, lakini ameshindwa kuweka bayana kitu kinachoifanya Rwanda kutumia zaidi bandari ya Mombasa. Anashindwa kusema kuwa miundombinu ndio chanzo; protokali za kisiasa zinambana.
 
Kwa aina hii ya usafiri wa reli huko India sidhani kama watafanya lolote jipya hapa kwetu.

Nimechungulia hiyo attachment, kusema kweli usafiri wa treni nchini India ni balaa.
Na hawa ndio tuliowapa dhamana ya kuliendesha shirika letu la reli!
Sijui kama tutafika, kwa sababu nilisikia mkuu EL akiwakataza kutofunga reli ya Tanga-Dar, kwani walikuwa wako mbioni kuifunga.
 
Mkwamo wa ujenzi wa hili daraja pengine Zitto (na waKGM wengine) wanaweza kutuambia mengi yaliyofichika.

Nimewahi kusikia kikwazo ilikuwa TRC wakidhani ujenzi wake ungepunguza mapato kwa shirika (myopiaism). Kama kweli mtazamo ulikuwa huu basi tusahau maana wameingia TRL (Indian) ambao ndio wenyewe kucheza na corruption.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…