Kigwangala afunguka sakata la kujivinjari na Pisi Kali Mbugani, amkana Poshy Queen: "Simjui, Sijawahi tembea na yule binti"

Kigwangala afunguka sakata la kujivinjari na Pisi Kali Mbugani, amkana Poshy Queen: "Simjui, Sijawahi tembea na yule binti"

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Unakumbuka sakata la mrembo Jacqueline Obeid a.k.a Poshy Queen na Hamisi Kigwangala?

Sasa Mwanasiasa Hamisi Kigwangala amezungumzia tuhuma zilizomwandama kuhusu mrembo Poshy Queen na pisi kali alizowahi kudaiwa kuzipandisha ndege na kwenda kujivinjari nazo mbugani kipindi ni Waziri wa Maliasili na Utalii. Katika mahojiano, Kigwangala amesisitiza kwamba "Sijawahi kutembea na yule binti, sijawahi kukaa naye meza moja, simjui literally"

Kigwangala alikuwa akieleza maono yake ya Wizara ya Maliasili na Utalii, akisema kuwa wazo la Urithi lilikuwa ni mpango mkubwa wa kuvuna pesa za kigeni kupitia makumbusho Dodoma na kuleta manufaa katika uchumi wa nchi.

"Urithi was a big concept kuliko zile blaa! blaa! Sasa watu wakaanza kusema Kigwangala kapanda na pisi kali kwenye ndege kaenda kutalii nazo. Kigwangala kamchukua Poshy Queen. Sasa ukimuangalia yule binti na umri wa Kigwangala unasema hii itakuwa kweli? Mwamba amepiga hapa. Sijawahi kutembea na yule binti, sijawahi kukaa naye meza moja, simjui literally."

Pia soma Dkt. Kigwangalla: Niliandika barua ya kujiuzulu Uwaziri baada ya kuona mambo hayaendi Wizarani
 
Kwa sasa apumzike tu. Zama zimeshampita, akafanye mambo mengine tu.
 
Back
Top Bottom