Kigwangala alikerwa pia na Mo kumpigia kampeni Rais siku ya Simba day?

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Ninaona wafuasi wake wengi ni pamoja na hao waliokerwa na kitendo cha Mo kumpa shavu Rais Magufuli pale uwanjani.

Hii chuki ya Kigwa iko juu kiasi kwamba baadhi ya watu tumeanza kuhisi huyu jamaa ana agenda ya siri na siyo hiyo 20B.
Kwani maelezo yanajitosheleza sana kuhusu kwa nini hiyo 20B haijawekwa.

Nikifuatilia akaunti yake ya tweeter,namuona kigwa ni mtu mwenye busara ndogo sana.Labda alifaulu mitihani kwa sababu ya uwezo wa kukumbuka tu(siyo akili maana hata kasuku anao huo uwezo wa kukumbuka sauti ila hana akili hata ya kumfikia mbwa)

Wasomi wawe wanajitafakari na wawe wanatumia mantiki,na siyo kiburi cha vyeti ambavyo mtu anaweza kuvipata hata kwa wizi wa mitihani.Sio kujiona umesoma na unaanza kuwashambulia waliofanikiwa kiuchumi.

Si mara ya kwanza kwa kigwa kushambulia personalities.Aliwahi kumshambulia Dr Mwaka kisa tu,ni yale mafanikio yake katika kazi ya tiba.

Amejichafua sana na naamini wana Simba wa Nzega,anawakwaza pia
 
Halafu inaonekana wewe ni mmoja wa wafuasi wa kigwa kule tweeter mnaoshangilia Mo kukomolewa eti tu kwa vile alimpigia kampeni Magu.

Kampeni imeingiaje kwenye 20B.
Aliyekutuma umekosea gear ya kuanza nayo.
 
Mo mjanja mjanja, sasa hivi naona anatafuta sympathy ya Raisi wetu kwa kujipendekeza kumpigia kampeni, Raisi wetu alishasemaga yeye ni mtetezi wa wanyonge, hawezikuona wazee waliopambana club wakinyanyasika na kutapeliwa na mtu mmoja anajisifu bilionea na kutumia hiyo status kuwaibia wanyonge.
 
Hao wazee ni kina nani?Ndo wanataka kugawana hizo 20B?

Kama babu yako ni maskini,usitarajie aje kuponea umaskini wake kwenye timu.
Simba ni ya wanachama na si wazee kama unavyodai.Huyo Kigwa uanachama wake haufiki hata miaka 7.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…