Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Maneno ya Mbunge Kigwangala kwamba kumsifia Rais ni uzalendo wa kwanza ni maneno ya kusikitisha yanayatuonyesha ni watu wa ajabu jinsi gani wanaotungoza wakati mwingine. Huyu ni mtu aliyekuwa waziri kamili na kutaka pia kuwa Rais wa taifa hili lakini hata huelewei kwamba nchi yake ni Jamuhuri na sio Ufalme!
Mtu aliye karibu na Kigwangala amuambie na amfafanulie kwamba uzalendo wa kwanza katika jamuhuri unapaswa kuwa katiba ya taifa.
====
Mtu aliye karibu na Kigwangala amuambie na amfafanulie kwamba uzalendo wa kwanza katika jamuhuri unapaswa kuwa katiba ya taifa.
====
Pia soma: Bunge siyo sehemu ya kumwagiana sifa wala uwanja wa kampeni, mnatia aibu!