Sasa ka analima afu mnagawana mavuno kuna shida gani?mkuu, kila kitu kina taratibu zake, ni sawa na mtu aje kulima shamba lako bila kukulipa chochote na wewe ufurahi eti kwa sababu ulishindwa kulilima. huo ni upumbavu.
mkuu, kila kitu kina taratibu zake, ni sawa na mtu aje kulima shamba lako bila kukulipa chochote na wewe ufurahi eti kwa sababu ulishindwa kulilima. huo ni upumbavu.Simba sio ya wananchi ni ya wanachama, lete katiba ya Simba iliposema Simba ni ya wananchi. Au mnafikiri hata mashabiki wa simba ni sawa na Utopolo wanaoambia timu ya wananchi wakati kwenye katiba zao wamesema ni ya wanachama.
Wenye Simba ni wale wenye kadi na wanazilipia kadi za Simba hao ndo wenye Simba maana ndo sifa ya kua mwanachama.
Furaha ya mashabiki wa simba ni kuona timu inafanya vizuri haijalishi inamilikiwa na nani. Hata kama atapewa hisa zote haina shida maadam brand ya Simba inaendelea kua juu
...πππView attachment 1559832
Dah....Mo amewadharu sana!π€£π€£
Bakheresa hawezi kununua hisa za Simba Kisheria,Sheria za Fifa haziruhusu mtu mmoja kuwa mmiliki wa Timu mbili kwenye Ligi Moja.Ninavyojua.
Huko nyuma Simba ilikuwa na hali mbaya sana.
Wataalamu wakaamuwa kutafutwe muwekezaji.
Akapatikana MO na Bahresa.
Akachaguliwa MO kwa baraka zote za kiserikali.
MO akaanza mchakato wa kuwekeza Simba, wakati huohuo akaanza kuihudumia timu ya Simba na kujenga miundombinu ya maendeleo kama uwanja nk.
MO ameulizwa mara nyingi sana, ni lini anaweka B20 za hisa zake asilimia 49.
Na amejibu mara nyingi sana kuwa mchakato bado haujakamilika na ukikamilika ataiweka hiyo B20.
Hizi ghalama anazozitumia ziko nje ya hiyo B20. Ni kwamba tu anaihudumia timu huku akisubiri soko la hisa la Simba lifunguliwe ili wadau wa Simba wanunue hisa za Simba kwenye ile 51% na yeye aweke hiyo B20.
Watu wanajiuliza vipi kama hataweka hiyo
B20.
Mchakato ukikamilika kama hata weka hiyo B20 basi hatua nyingine zitafuatwa, hatua za kisheria, kwamba mkataba unasemaje kama mwekezaji kashindwa kuweka pesa katika kipindi husika, hatua zipi zichukuliwe, hapo sheria itachukua mkondo wake.
Lakini jibu rahisi ni kwamba, Simba itauza zile hisa za uwekezaji za 49% kwa mwekezaji mwingine. Yaani itarudi kwa mwombaji wa pili Bwana Bahresa kumsikiliza kama nia yake ya kuwekeza Simba bado ipo au la.
Kama atakubali atapewa timu, la akikataa atakaribishwa mwekezaji mwingine.
Kwa sasa timu imetulia na inahudumiwa kila kitu na mtia nia MO. Basi tuendelee kusubiri mchakato ukamilike.
Kama kuna mashaka basi watu wa kwanza wa kuwauliza ni managementi ya Simba. Kuwashauri waitishe kikao cha wadau wa Simba na ajenda iwekwe mezani ili ijadiliwe kwa kina na kutoa suluhisho.
Sisi wadau wa Simba Sport lazima tuiamini management tuliyoiweka, ndio maana wapo hapo ili wafanye maamuzi kwa niaba ya Wadau wa Simba na Mwekezaji.
Kuhoji sio kosa na kama mtu anahoja flani basi afuate utaratibu wa kuhoji, kuhoji kwa kushinikiza majibu nje ya vikao vya Simba hakuta leta tija.
Ni kuidharau management ya Simba ambayo imewekwa kwa kufuata taratibu stahiki, na kukaribisha sintofahamu ambayo sio
ya lazima.
Nadhani kila taasisi ina namna yake ya kujiendesha. Na kama mtu anamashaka kuna namna yake ya kueleza mashaka yake.
Kama kila anaye jisikia kuuliza maswala ya Simba, anauliza mahali popote na kutaka majibu, itakuwa ni vurugu mechi tu.
Haujui Mpira wa Tanzania wewe! Wangapi wamefilisika kwa ajili ya mpira? Soka la bongo halina faida hiyo unayosema GSM mpaka leo wanahamgaika na mauzo ya jezi.Simba tunatumika kumuingizia kipato Mudi bila kujua, hajatuwekea senti zetu ila kila mali yetu kuna nembo za Mudi. Hahahaaaaa umaskini ni upofu wa kudumu.
Naona hili suala ni nyeti ila kwa vile kipofu huwa haoni anakokwenda ngoja tutulie maana shimo la mauti linakaribia
Basi tutamtafuta mwekezaji mwingine wala haina shida.Bakheresa hawezi kununua hisa za Simba Kisheria,Sheria za Fifa haziruhusu mtu mmoja kuwa mmiliki wa Timu mbili kwenye Ligi Moja.
Tatizo hizo hela anazotoa sasa hivi huo unaoita msaada upo kwenye maandishi Kisheria maana asije hapo baadae akataka arudishiwe gharama zake.Basi tutamtafuta mwekezaji mwingine wala haina shida.
Ila kwasasa msaada anaoutoa MO kwa Simba ni muhimi sana na wadau wa Simba tunafurahia matunda yake.
Mfano akiihudumia hivi miaka kumi au kumi na tano na kuamua kuondoka, Simba itakuwa ktk hali ya juu kimapato na kimaendeleo na atakuwa ametumia zaidi ya hiyo B20.
Halafu lazima watu wajue, hiyo B20 ni ya MO mwenyewe awe ameiweka pale Simba au la.
Hata akiiweka leo anaweza kuiondoa vile vile maana sheria inamruhusu, au akaiuza kwa mtu mwingine maana ni hisa yake binafsi.
B20 inabaki kuwa pesa yake, na lazima aiweke katika mazingira anayo yaamini kuwa hayatampa hasara. Ndio maana anahakikisha watu atakao fanya nao kazi ya kuizalisha pesa yake wawe anaowaamini.
Ili uweke mtaji wako lazima uhakikishe mazingira ni rafiki na hayahatarishi faida unayoitarajia.
Nipo.
Sent from my MI MAX 2 using JamiiForums mobile app
Nimeona baadhi ya wachambuzi maandazi wamepata jambo la kuongelea wiki hii nzima baada ya Kigwangala kuhoji uteuzi wa CEO mpya wa Simba.
Kifupi tu namuomba aache kuleta uswahili na choko choko kwa club ya Simba kwani naamini ukitoa dili zilizomtoa kisiasa, hana uwezo wa kujua masuala ya uendeshaji timu, uongozi na usimamizi wa miradi mikubwa.
Kama tu ameshindwa tu kuimarisha chuo chake, mradi ambao ni uwekezaji wenye faida kubwa na wenye uwezo wa kuajiri watu wengi, atakuwa na mawazo gani ya kuishauri Simba kama sio tu kuanzisha choko choko?
Katamka sio mara moja na sio mara mbili kuwa huduma anayoitoa kwa sasa ni ya ufadhili tu kwakuwa naye anatangaza biashara zake kupitia Simba.Tatizo hizo hela anazotoa sasa hivi huo unaoita msaada upo kwenye maandishi Kisheria maana asije hapo baadae akataka arudishiwe gharama zake.