the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Dr. Hamis Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa X ameandika
Mhe. Lissu hatoboi huu uchaguzi. Last two weeks akizungumza kwenye Space/Clubhouse nilimsikia akisema yeye hatoondoka CHADEMA, namnukuu “I ain’t going nowhere…” Akasema tena situation yake na ya Mhe. Zitto ziko tofauti sana, akidai kuwa yeye amejaza fomu kuomba nafasi wakati Zitto alishughulikiwa kwa kufuata ‘disciplinary proceedings’ za chama kwa tuhuma za usaliti na mapinduzi, yaliyoitwa MM, akiwa na akina Kitila etc.
Maneno haya yamefanya nizame kujikumbusha namna walivyoshughulika na ndugu yangu.
Nikakutana na post ya Zitto yenye maneno ya maumivu makali na hasira nzito! Nikakumbuka nilivyomhurumia sana. Zitto was a shining star in Tanzanian political landscape, he was a role model to many youngsters, lakini wenzake waliamua kuizima nyota ile! Same way Zitto inspired many, ndivyo ambavyo Vijana wengi walipenda upinzani kufuatia siasa za chopa za Mbowe na baadaye Ubishi wa Lissu bungeni na detailed hoja za Dr. Slaa. Story for another day.
Uchaguzi ukiisha kaka Lissu atapelekwa kwenye disciplinary proceedings, kabla hazijaisha, atahama mwenyewe maana hawezi kupata haki dhidi ya comrades aliowatukana na kuwachafua. Attack dogs watamshambulia kama yeye alivyomshambulia Zitto.
Karma itakuwa inafanya kazi yake. Lissu Atabaki helpless peke yake na mikutano yake ya clubhouse/Space! Hii ndiyo siasa sasa. Siasa ni mchezo wa ajabu, lakini pia ni darasa kubwa la maisha. Somo la karma litakuwa linamuingia. Miaka takribani kumi iliyopita, tuliwashuhudia Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu wakiongoza juhudi za kumtoa Mhe. Zitto Kabwe ndani ya CHADEMA.
Tukio hilo lilikuwa na matukio ya kusikitisha, huku Mhe. Lissu akichukua nafasi ya kumshambulia Zitto vikali kwa niaba ya Mhe. Mbowe.Kwa wengi, kipindi hicho kilionekana kama mwisho wa Zitto kisiasa. Hotuba na maneno makali ya Mhe. Lissu yalisambazwa kwa kasi, yakiwa na nia ya kumdhoofisha Zitto. Lakini Zitto hakufa kisiasa, aliibuka na ACT-Wazalendo, chama kinachopigania nafasi kubwa kwenye siasa za nchi hii hadi leo.Cha kushangaza ni kwamba leo, miaka michache baadaye, karma imeleta sura mpya kwenye siasa hizi.
Mhe. Lissu sasa ni mkosoaji mkubwa wa Mhe. Mbowe, akimshutumu kwa ukosefu wa demokrasia ndani ya CHADEMA. Aliyekuwa mtetezi wa Mbowe amegeuka kuwa mkosoaji wake mkubwa, na chama hicho kiko kwenye mgawanyiko wa wazi.
Historia inaonekana kujirudia, lakini kwa sura tofauti.Hii ni funzo kubwa kwa wanasiasa wetu: tusifanye dhuluma kwa wengine tukijiamini kwamba sisi ni salama. Leo ni wao, lakini kesho inaweza kuwa zamu yetu.
Haki na busara ni misingi ya siasa bora.Kwa ujumla, historia ya siasa za nchi yetu inatufundisha kuwa kila tukio lina matokeo yake. Matendo ya jana yanatengeneza mazingira ya leo. Hali inayojiri ndani ya CHADEMA inatufundisha thamani ya umoja, uvumilivu, na kuheshimiana katika siasa zetu. Karma haikosei, na leo tunaiona ikitekeleza kazi yake.
Lissu ataweza kuja CCM, ama ataenda ACT? Ama CUF ama NCCR? #HK #Fighter #NjeYaBox
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025