Kigwangalla asema kukataza mabegi ya shangazi kaja kwenye treni ya SGR ni ubaguzi wa wazi

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Kigwangala aandika haya katika ukurasa wake wa X;

Hii ni aina ya mambo ambayo hatuwezi kunyamaza. Ni aina ya mambo yenye viashiria vya ‘ubaguzi’ wa wazi.

State crafting inataka kulinda tunu zilizoasisi Taifa. Mojawapo muhimu na kubwa ni usawa, na inclusion. Hata siku moja tusithubutu kuruhusu ama kufanya mambo yanayoigawa nchi na kuzishambulia tunu za Taifa letu kama usawa.

Yeyote anayejaribu kuwabagua wananchi wenzetu ambao bado wapo kwenye hali ya chini ya uchumi kwa namna yoyote ile tumkemee. Hatutakii mema.

SGR ni mali ya watanzania wote bila kujali hali zao na shughuli zao wanazofanya, siyo mali ya wasomi na washua tu, hata wauza kuku inawahusu.

Juzi nilitoka na mama yangu mzazi kwenda lunch pale Montana, Millenium towers, mama akanikumbusha story ya utotoni mwangu nikienda kuwasalimu baba zangu kule Goweko Mlimani nikipewa zawadi ya kuku na Shangazi zangu. Hivi leo unategemea mwanangu akienda kule akapewa zawadi ya kuku na babu zake amuache kweli?

Ukisoma autobiography ya Lee Kuan Yew, From Third World to First, The Singapore Story, anaeleza walipojenga flats na watu wakawa wanahamishwa na serikali kutoka kwenye squatters kwenda kwenye hizo flats, walikuwa wanapanda kwenye lift na ng’ombe wao! Hawakuzuiliwa. Washua waligundua ni kazi ngumu sana kukitoa kijiji kichwani, wali-accommodate mahitaji ya warugaruga. They didn’t condemn.

Taifa hujengwa namna hii sasa. Tuendelee lakini tusimuache mtu nyuma. Tujitahidi kuweka mifumo na miundo itakayowezesha kila mmoja wetu kufaidi mema ya nchi kwa urefu wa ukamba wake.

Unajua kwa nini kila anayetoboa kutoka usweken anaanza kujenga ukuta wa fence kabla hata ya nyumba, baadaye akihamia anaongezea electric fencing, CCTV cameras, security company kwa ajili ya rapid response, ananunua silaha zake anaweka chini ya mto, anafuga na German shepherds wakali, na bado kwenye milango na madirisha ameweka vyuma? Equity! Equity! Equity…my countrymen! Tuishi na wengine waishi…ukiwa na maguvu ya kumzaba mtu makofi, muachie haki yake ya kulia. Fairness! Fairness! Fairness! That’s the name of the game.
 
Aache blahblah

Huo mradi wautunze maana wabongo wanajulikana kwa kuharibu mali ustaarabu sifuri

Ova
Nakubaliana na uharibifu wa wabongo. Ila naona kama vile huu mradi wa train unaenda kugeuzwa kuwa ni usafiri fulani wa kishua tofauti na lengo la awali la awali.
Tuna shida ya kuanza kujenga vitu halafu vikiisha ndipo tunakuja na plan ya kuvirun au tunabadilisha plan ya mwanzo baada ya kukamilika. Nilidhani train italeta gharama nafuu za kusafirisha raia kuliko mabasi naona ni kitu tofauti basi litabaki kuwa nafuu.
 
Waweke madaraja watu wakae kwa madaraja,mbona hata treni ya tazara zamani ilikuwepo first class,second, third

Ova
 
Kigwangwala analazimisha ku trend tu mitandaoni
 
Kinachotokea ni sawa na mbeba zege apakie kwenye Mercedes Benz kwenda kibaruani. Nani anabeba gharama?

TRL wanajua hali ya kiuchumi ya Watanzania, sasa kwanini wamenunua mabehewa ya bei mbaya, ya luxury, yasiyoendana na hali za watumiaji?
 
Kinachotokea ni sawa na mbeba zege apakie kwenye Mercedes Benz kwenda kibaruani. Nani anabeba gharama?

TRL wanajua hali ya kiuchumi ya Watanzania, sasa kwanini wamenunua mabehewa ya bei mbaya, ya luxury, yasiyoendana na hali za watumiaji?
Nimekumbuka zile train za wahindi. Wahindi wanadandia ahdi juu yale ni maajabu kabisa. Sema tu waweke utaratibu mzuri usafiri wa train uwe cheap otherwise ukiendelea kuwa wa luxury kama wanavyotaka kuufanya nadhani hilo halikuwa lengo lake.
 
kila baishara inatakiwa kuwa unique .waboreshe na treni za zamani na mizigo na hiyo express hiwe kivyake na mabasi yawe kivyake.
ila wameniuzi nimeenda na makande kwenye SGR na hotpot langu kubwa wamenikatalia wanasema bado wamepeleka mswaada bungeni kuhusu makande
 
Nimekumbuka zile train za wahindi. Wahindi wanadandia ahdi juu yale ni maajabu kabisa. Sema tu waweke utaratibu mzuri usafiri wa train uwe cheap otherwise ukiendelea kuwa wa luxury kama wanavyotaka kuufanya nadhani hilo halikuwa lengo lake.
Halikuwa lengo lao kivipi? Huo ni upigaji tu. Walishindwa nini kununua mabehewa yanayoendana na vipato vya Watanzania?
 
Watanzania hatuelewi tunataka nini, unabebaje kuku na shangazi kaja kwenye train? Ustaarabu ni neno gumu Sana Kwa watanzania
Hata kwenye mabasi hadi mbuzi walikua wanabebwa ila kadri muda unavyozidi kwenda mambo hubadirika.

Hata hiyo sgr wameanzia mbali sana kukataza hata shangazi kaja, hiyo sio sawa.
 
Aache blahblah

Huo mradi wautunze maana wabongo wanajulikana kwa kuharibu mali ustaarabu sifuri

Ova
Wote NI walipa Kodi mkuu huo mradi haukujengwa kwa ajiri ya wenye nacho Tu! Umesafiri kwenda kwa bab yako Bibi au mama wakakupa kuku kwa hiyo unaiacha kwa sababu usafiri hawaruhusu mambo ya namna hiyo ! SGR haikujengwa kwa ajiri ya watu flani wa kipato cha juu! Wewe ukisema hivo na wote NI walipa Kodi huoni kama tunapoelekea siko kabisa , mradi umejengwa usaidie watu wote kinachotakiwa nikuweka utaratibi mzuri MIZIGO kama hiyo ifanyiwe ufumbuzi katika ubebaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…