Kigwangalla asema kukataza mabegi ya shangazi kaja kwenye treni ya SGR ni ubaguzi wa wazi

Kigwangallah ni mtu aieelewa anataka nini,
 
Kwa hiyo manataka muingie na kuku,samaki wabichi kwenye train?
 
Pure
Shangazi kaja ina shida gani? Hapo kwenye Kuku sijui, ila mtu akibeba shangazi kaja kuna tatizo gani?
Shangazi kaja yana kelele sana yale mamifuko. Nadhani wametumia kigezo cha kelele ni uchafuzi wa mazingira kuyakataza.
 
"ukiwa na uwezo wa kumzaba mtu makofi, muachie haki yake ya kulia" mwisho wa kunukuu

Hili ni jambo fikirishi
 
Yaani Singapore watu walipanda na ng'ombe wao kwenye flats 😆 doh kigwa bhana akisha kaa kwenye LE yake nyeupe ile anacharaza tuu
 
sasa mtu katoka zake huko nzega, alikuja dsm kwasababu ya shule tu pale muhimbili, hajawahi kupanda hizo treni,hana exposure, unategemea angesemaje?
 
Hata kwenye mabasi hadi mbuzi walikua wanabebwa ila kadri muda unavyozidi kwenda mambo hubadirika.

Hata hiyo sgr wameanzia mbali sana kukataza hata shangazi kaja, hiyo sio sawa.
we sema upande basi la kivukoni, ukifanya mchezo mchuzi wa samaki wabichi wanaambukiza kwenye suruali, na unaenda ofisini.
 
Inaelekea mwisho wake mradi huu si mzuri, litakuwa li 'WHITE ELEPHANT' lisilo na tija!
 
Aache kujitafutia umaarufu kwa hoja za kijinga. Lazima tuzingatie standards ili mradi uweze kudumu na kuwa wa viwango wakati wote. Nawapongeza sana TRC kwa maamuzi haya!
 
Wangeweka utaratibu wa kupima mizigo halafu inakuja na treni ya Cargo au wangekata compartment moja ya mizigo mikubwa kwenye behewa mojawapo.

Nimeielewa sana mada.
 
Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangala yuko serious kutetea kuku, mbuzi, samaki na mazao kupakizwa kwenye treni ya abiria?

Itakuwa jambo la ajabu sana TRC kukubaliana na mawazo hayo ya ajabu ajabu ya mtu huyu kwani hata kwenye mabasi mengi siku hizi huwezi kusafirisha vitu hivyo na ukiwa na mzigo mkubwa hata kwenye buti unalipia.
 
SGR yenyewe haijaisha ila mijadala ya kipumbavu imeanza, Nchi masikini kama Tanzania yenye raia masikini utawatenganisha je na mifugo yao ambao ni source of income kwao, masikini akipata kitu muhimu watu watakoma tu...........
 
Hawa si ndo wale wanatembelea vietee?
 
Hamisi atakua amezowea kubeba kuku na mbuzi kwenye gari lake akienda kwa waganga wa kienyeji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…