Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
"Chama cha siasa huanzishwa kuwaleta pamoja watu wenye mawazo na sera zenye kufanana. Lengo kuu ni kuleta ustawi wa watu. CCM haikuahidi mchakato wa Katiba kwenye ilani, bali ustawi wa watu. Nakubaliana na Mhe. Rais, kwa sasa tukomae na ustawi wa uchumi, Katiba baadaye!"- Mh. Kigwangalla
===
Maneno zaidi ya Kigwangallah kutoka twitter
Wanasiasa wanaanzisha mjadala wa Katiba Mpya kukidhi matakwa ya kisiasa ya kwao binafsi na siyo hitajio la wananchi walio wengi.Katiba Mpya haiweki ugali mezani, wala dawa zahanati, inaweza kusubiri. CHADEMA watafute ajenda ya maendeleo ya watu, na siyo Katiba Mpya
Chama cha siasa huanzishwa kuwaleta pamoja watu wenye mawazo na sera zenye kufanana.Lengo kuu ni kuleta ustawi wa watu.CCM haikuahidi mchakato wa Katiba kwenye ilani,bali ustawi wa watu.Nakubaliana na Mhe.Rais, kwa sasa tukomae na ustawi wa uchumi, Katiba baadaye
Wanaodai Katiba Mpya leo ndiyo waliokimbia Bunge la Katiba.Walikimbia kitu gani na je walichokimbia kimeondoka ama kipo? Kama kipo, wana uhakika gani kwamba safari hii kitabadilika?Ama ni ajenda ya kisiasa tu kuwayumbisha wananchi na kujaribu kuchelewesha maendeleo?
Kama Katiba tuliyonayo imetuwezesha kuvuka kipindi kigumu cha msiba,na imetuwezesha kujenga barabara na kufikisha maji ya Ziwa Victoria Tabora, inafaa kuendelea nayo kwa muda mpaka hapo mahitaji ya kweli ya Katiba Mpya yatakapojitokeza.Tusikubali kutoka kwenye reli
Kuna watu wanadai kuwa Katiba Mpya inahitajika sasa hivi,sijui wameambiwa na wananchi wa wapi,maana mimi sijawahi kudaiwa na wananchi wa Nzega Vijijini ninaowawakilisha.Wao wananidai umeme,maji,barabara na shule. Kwa sasa tujikite na haya kwanza, Katiba baadaye.