Kigwangalla na chozi la mamba, kama ana uchungu wa kweli vile

Kigwangalla na chozi la mamba, kama ana uchungu wa kweli vile

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Ukiwakuta hawa wamevaa ma scarfs ya bendera ya taifa na kushikilia ilani ya CCM kwenye makwapa yao unaweza kusema hii nchi imebarikiwa sana.

Wengine walikwapua mabilioni ya wizara ya utalii na CAG akathibitisha lakini kimyaaaaa bado wanajifanya wazalendo, wakatumia hadi ndege za Tanapa kula bata na vimada lakini leo wanashadadia wanuka jasho wakamuliwe tozo eti zitajenga madarasa na zahanati.

kigwa.jpeg


Alichoandika Kigwangalla kwenye account yake ya twitter

Hivi kweli Wabongo wote tumeshindwa kuendesha biashara ya DART mpaka tumpe hii kazi kampuni ya nje, au kuna nini? Aibu yetu wallah! Yaani tumekopa, tumejenga halafu kuendesha ma-bus tu na kukusanya hela tumeshindwa! Sasa tutaweza biashara gani?

BRT kupunguza adha ya usafiri jijini Dar ambapo takriban watu 200,000 wanasafiri kila siku. Ila itaondoa barabarani daladala zaidi ya 8000! Ajira ngapi zitapotea? Fikiri kuhusu mnyororo: madereva, makondakta, gereji, maduka ya spares, mama ntilie, wenye ma-bus, sheli nk!

Wahandisi huwa wanaongea kuhusu ‘multi-modal’ design ya miradi. Toka 2013 nimekuwa nikiuliza hivi ni kwa nini kwenye BRT hawakuweka ‘provision’ ya reli nyepesi/‘tram’, na ni kwa nini miundombinu haifiki kwenye vituo vikubwa vya Uchukuzi kama station/bandarini/AirPort/stendi?

Wahandisi mnapo-design miradi muwe mnaalika wachumi wawasaidie la sivyo mtaendelea kutuangusha. Mf. Hivi ni kwa nini mli-design phase 1 ya SGR bila kuiingiza bandarini? Mkaishia stesheni tu. Inamaana hamkujua kuwa mizigo ndiyo biashara kubwa zaidi ya reli kuliko abiria?

Kama tunaona kampuni za ndani ama serikali haiwezi kuendesha kampuni ya BRT, itakuaje kwenye Shirika la ndege, meli na reli? Tutaweza? Hii wala siyo issue ya kisiasa, ni issue ya kiuchumi na ‘mindset’! Ni ya kwetu sote, ni ya kijamii kwa ujumla wake! Tujitafakari sana.
 
Kigwa ni mixer mnafiki nafiki hivi siyo wa kumwamini.
 
Tunamjadili mtu badala ya issue. Mradi unabinafsishwa na hapa tunaletewa hoja ya kumjadili anayehoji. Nani asiyejua kuwa Kigwangala ni rangi mbili? Nani asiyejua kama ni mnafiki?

Hebu tuwe siriaz kidogo..
 
Kigwa ni mixer mnafiki nafiki hivi siyo wa kumwamini .
Tangu nikutanae nae anakimbia barabarani sijui mazoezi na jua la saaa Saba kwake sijui Mbezi beach baada ya kutumbuliwa nikamuona ana furazuturesheni za kukosa kosa ulaji ulaji. kwa Ivo apuuzwe tu.
 
Yaani Bashe na Kigwa huwezi kusema wametoka mkoa mmoja.

Bashe IQ kubwa, lakini huyo yeye Mademu tu anachowaza
 
Mwananchi anastahili kuteseka,kwasababu ngoja kampeni zianze, apewe khanga kofia na tisheti utamuona anavyokata kiuno
Mbona wewe unakataka viuno humu kumsifia rais wako mpendwa
 
Kuacha udhaifu na matendo yake huyu bwana kaleta hoja ya msingi yenye maslahi kwa umma Cha kushangaza GT wameacha kujadili hoja wanamjadili mtu

"Akili kubwa hujadili hoja akili ya wastani hujadili matukio akili ya chini kabisa hujadili watu" Socrates

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom