EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Vita ya kwanza ya dunia iliibuka kutokana na kuwepo kwa mataifa (multipolar) yenye nguvu ya kiuchumi na kijeshi yaliyokosa kuheshimiana! Baada ya vita hiyo, kukatengenezwa 'the league of nations' kama njia ya kutengeneza utengemano kati ya mataifa hayo!
Hata hivyo, vita hiyo haikuwa fundisho kwa nchi hizo na hali hiyo ya kutoheshimiana ikaja kuzua vita ya pili ya dunia iliyosaidia kutokomeza hali ya uwepo wa nchi kadhaa (multipolar) zenye nguvu za kiushindani na kuja kuunda (bipolar) pande mbili zenye nguvu za kiushindani; Marekani na NATO yake dhidi ya USSR!
Pande hizi mbili zilidumu huku zikifanikiwa kuigawa dunia kwenye kambi mbili huku sehemu fulani ya nchi zikiamua kutofungamana na upande wowote!
Marekani na NATO yake, ilijisahau kwamba chanzo cha vita mbili kubwa zilizopita ni kukosekana kwa kuheshimiana na kila nchi kutaka kuwa juu ya zingine!
Hivyo, katika kujisahau huko NATO ambayo inajinadi kuwa ni umoja wa kiulinzi na usalama kwa nchi wanachama; ilijipa majukumu ya kuhakikisha kwamba ushawishi wa USSR haupanuki duniani huku yenyewe ikijipa mamlaka ya kutandawaa katika kila kona ya dunia na kuifanya kila nchi iliyoenda kinyume na matakwa yake ikandamizwe na kufikia kuja kupige magoti na kunyenyekea kwayo!
Marekani na NATO yake haikuamini katika uwepo wa kambi mbili shindani duniani zaidi ya kutamani kuiona USSR ikisambaratika na kuifanya Marekani chini ya kivuli cha NATO ibaki kuwa (Unipolar) mtawala pekee mwenye nguvu duniani!
Jitihada hizo za Marekani kwa msaada wa NATO, za kutaka kuitawala dunia zilikuja kuzaa matunda mara baada ya USSR kuja kusambararika 1991!
Baada ya kubaki kambi moja la Marekani kama mtawala pekee mwenye nguvu ya kuinyoosha dunia kadili itakavyo, ndipo sasa nchi hiyo ilipoanza kuisukuma dunia katika kufuata kile kilichoitwa 'USA Liberal Democracy' na kuzitaka nchi mbalimbali kubadili mfumo wa kiutawala na kuja kufuata mfumo huo!
Kupitia harakati hizi za kusambaza mageuzi ya kimfumo duniani, Marekani ilifanikiwa kutengeneza vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi kadhaa, kuzibana kiuchumi na kuzisukuma kwenye kuzibebesha mizigo ya madeni kupitia mikopo ya benki ya dunia ambayo Marekani ndiyo inayoshika sehemu kubwa ya hisa zake na kufanya rais wa benki hiyo kuwa ni lazima hawe ni mmarekani na anayechaguliwa na rais wa Marekani; na pia ikiwa na 17% ya kura katika IMF ambayo kwa kawaida rais wake huwa ni wa kutoka Ulaya!
Mzigo huo wa madeni haukuziathiri nchi za Afrika na Asia tu bali hata nchi za Ulaya zilizo wanachama wa NATO pia zilijikuta zikiwemo kwenye kitanzi hicho!
Kwa mfano; nchi kama Ureno, Italia, Ireland, Ugiriki na Ispania hazikusalimika katika msukosuko wa mzigo wa madeni!
Mbali na hayo, Marekani iliweza kupandikiza vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi zisizo tii matakwa yake, kufadhili vikundi vya waasi, kutengeneza asasi zisizo za kiserikali (NGOs) zenye mlengo wa kupenyeza misigano ndani ya nchi nk!
Mbali na kuutawala dunia kwa namna zote, bado Marekani ilionekana wazi kwamba haikutosheka na hali hiyo zaidi ya kutaka kuona nchi kama China, Iran, Korea kaskazini na hususan Urusi; zote zikinyong'onyea na kuitii kama kiranja wa dunia!
Marekani ilisambaza makambi yake ya kijeshi kwenye kila kona ya dunia, NATO nayo ikaanza kujipanua bila kuheshimiana na Urusi, vitisho, vikwazo, kuangushwa kwa tawala ndani ya nchi mbalimbali duniani mfano, Iraq, Libya, Misri nk ikaja kuwa ndio mtindo wa kambi la magharibi!
Urusi chini ya mwamba Vladimir Putin iliona hatari inayotengenezwa na kambi la NATO na hivyo ikaona wazi kwamba wakati wa kuikumbusha kambi hiyo kwamba kuna haja ya kuheshimiana na kuthamini uhuru na mamlaka za nchi mbalimbali umefika!
Ikaanza kwa kuizuia Marekani na washirika wake kumuondoa rais Bashar al Assad huko Syria! Haikuishia hapo bali ikaenda kumbakisha madarakani Niclas Maduro aliyekuwa akiandamwa na kambi la magharibi huko Venezuela na haikusita kutia mguu kwenye nchi za Afrika kwenda kukabiliana na makundi ya uasi yanayofadhiliwa na nchi za magharibi!
Tamaa hiyo ya Marekani na NATO yake ya kutaka kuwa 'Unipolar' milele matokeo yake imeipelekea nchi hiyo kuingia pabaya huko Ukraine na kuikologa 'ndonya' Urusi; ambayo nayo katika kuionesha NATO kwamba sasa imetosha na tunakwenda kuufumua mfumo mzima wa 'unipolar' na kutengeneza mfumo mwingine wa 'multipolar' ambao hautoruhusu tena nchi moja ama mbili kutawala dunia; zaidi ya kufungua milango kwa nchi mbalimbali zenye nguvu kuweza kushika hatamu za kutawala pasina kuoneana ama kuonewa na nchi moja!
Kinachoendelea huko Ukraine ni sehemu ya harakati za kuiondoa dunia katika mfumo wa 'unipolar' unaoibeba Marekani pekee na kuja kusimika mfumo wa 'multipolar' ambao nyuma yake nchi mbalimbali kama Korea kaskazini, Iran, Brazil, Afrika kusini, China, India, Urusi na nyinginezo nyingi zitapata fursa ya kujisimamia na kujiondoa kwenye kuendeshwa na nchi moja!
Hivyo, wakati haya yakiendelea, Afrika isibaki nyuma!!