Kihingo, Kenya: Wabunge wagoma kukaa kwenye viti vya plastiki, mkutano waendeshwa wakiwa wamesimama wima

Kihingo, Kenya: Wabunge wagoma kukaa kwenye viti vya plastiki, mkutano waendeshwa wakiwa wamesimama wima

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
wamesimama.jpg

Baadhi ya wabunge wa Bunge la Wawakilishi Kaunti ya Kihingo nchini Kenya, wamelazimika kuendesha mkutano wao wakiwa wamesimama ikiwa ni hatua yao ya kugoma kuketi kwenye viti vya plastiki katika ukumbi wao wa mikutano.

Wanasiasa hao ambao wamekuwa wakitumia viti hivyo tangu wachaguliwe takriban miezi saba sasa baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya kutokana na ukarabati wa ukumbi wao wa mikutano, wameeleza kuchoshwa na hali hiyo.
Wabunge hao kutoka Kihingo iliyoko kusini-magharibi mwa Kenya wamedai kuchoshwa na hali hiyo na mmoja wao, Antony Rotich anasema ni jambo la aibu jamii kushuhudia watunga sheria wao wakiwa wameketi kwenye viti vya plastiki.

Spika wa Bunge hilo la Wawakilishi, Philip Wanjohi, amezungumzia hali hiyo na kusema wawakilishi hao wa Bunge la Kaunti (MCAs) wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu kutimiza wajibu wao wakiwa kwenye viti hivyo vya plastiki.
“Tumeteseka kwa muda mrefu. Tunashangaa na kujiuliza ni kwa nini kuna ujenzi unaendelea katika maeneo mengine ndani ya eneo la Bunge lakini ukumbi wa wawakilishi ujenzi wake unasuasua mno licha ya kuanza kwake mwaka mmoja uliopita,” alisema mwakilishi kutoka Kihingo, George Kiere.

Awali, wawakilishi hao walipanga kugoma kushiriki mkutano wao hadi pale walipopewa ufafanuzi na kiongozi wao, hapo ndipo angalau wameshiriki wakiwa wamesimama.
Kumekuwa na taarifa kuhusu msuguano kati ya wawakilishi hao na uongozi wa bunge lao kuhusu kusuasua kwa ujenzi huo.

“Uhusiano kati ya ofisi ya katibu wa bunge na wawakilishi si mzuri. Kamati husika imeshindwa kutoa maelezo kuhusu hali hiyo,” anasema kiongozi wa wachache kwenye bunge hilo, Peter Palang’a.

Chanzo: Tanzanite timeshttp://tanzanianewsroom.com/wabunge-wagoma-kuketi-kwenye-viti-vya-plastiki-mkutano-waendeshwa-wima/
 
Back
Top Bottom