Kihongosi: Baadhi ya Mila na Tamaduni zinachangia Kipindupindu Simiyu

Kihongosi: Baadhi ya Mila na Tamaduni zinachangia Kipindupindu Simiyu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Akizungumzia taarifa za uwepo wa Kipindupindu Mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amesema Viongozi wanatakiwa kushirikiana na Jamii katika kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu suala la afya na matatizo mengine yanayogusa maisha ya watu.

Amesema “Hatuna kesi ya Watu waliofariki kwa Ugonjwa wa Kipindupindu lakini ninamaamini baada ya WHO kufika, Serikali walituma Watu wa Wizara, tunaamini ndani ya muda mfupi jambo hili litaisha.

Wananchi wazingatie hatua zote za msingi ambazo wanaelimishwa na Watu wa Afya kwani katika vitu vinavyochangia Uwepo wa Ugonjwa wa Kipindupindu ni baadhi ya Mila na Tamaduni za kwetu ndani ya Simiyu na uelewa mdogo wa Wananchi kuhusu suala hilo, pia tumewaelimisha Wananchi kujenga vyoo.

Chanzo: PBTV

Pia soma
~ Kipindupindu Simiyu kimeshamiri, kinaua ni hatari! Mbona Serikali haiweki wazi 'status' ipoje?

~ Wataalam wa Afya waingia mtaani kufanya jitihada za kudhibiti magonjwa ya kuhara Mkoani Simiyu
 
Back
Top Bottom