Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Washwahili wengi hatujui matumizi ya "which" na "that" katika kiingereza. Kwa vile maneno hayo yanaweza kuwa na maana moja katika kiswahili, basi huwa tunependa sana kutumia "which" hata mahala ambapo ni pa "that." Maneno hayo japo yote yananuganisha vipande viwili vya sentence
huleta maana mbili tofauti kama ifautavyo.
Fikiria sentensi hizi za kiswahili:
(1) Nyumba yangu, ambayo ina milango mitano, iko kwenye kitongoji cha Kariakoo. Sentensi hii maana yake kubwa ni kuwa nyumba Yangu iko kwenye kitongoji cha Kariakoo, ila ninaongezea kueleza kuwa nyumba hiyo ina milango vitano, lakini ingeweza kuwa na milango sita, nyumba ni ile ile.
(2) Nyumba yangu yenye milango mitano iko kwenye kitongoji cha kariakoo. Sentensi hii ina maana kubwa ni kuwa nyumba yangu ya yenye milango mitano iko Kariakoo; hii inassisitiza kuwa ni nyumba yenye milango mitano, siyo tofauti na hapo..
Sentence ya kwanza ndiyo itayoandikwa kwa kiingereza kuw "My house, which has five doors, is located in the Kariakoo suburb", na ile sentence ya pili itaandikwa kwa kiiengereza kuwa "My house that has five doors is located in the Kariakoo suburb." Sentensi hizi zina maana tofauti kabisa kwa msikilizaji wako wa kiingereza.