Kiingereza, Kifaransa, Kidutch, Kijapan, Kichina; Wapi Kiswahili?

Guus

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
1,139
Reaction score
842
Bandugu,
Nilikuwa napitia wavuti ya TANAPA ili nijipatie habari mbili tatu za kujifunza, nikashangazwa na hii taasisi yenye kupigia upatu utalii wa ndani kutoweka lugha ya Kiswahili katika wavuti yao. Kwenye uchaguzi wa lugha, nimeona wameweka lugha za Kimataifa kama nilivyoorodhesha katika kichwa cha habari. Hapa nikapata wazo kuangalia wavuti nyingine za Setikali, nazo pia zimejikita katika lugha ya Kiingereza. Binafsi sioni ubaya wa kutumia hizi lugha za Kimataifa, shida yangu ni kwa nini katika mibadala ya hizo lugha Kiswahili kisiwapo!? Ndiyo, inawezekana wengi wa watumiaji wa mitandao ni watu wenye uelewa wa lugha hizi za Kimataifa (ingawa sina hakika) lakini hatudhani kuwa kujumuisha lugha ya Kiswahili kungeongeza watumiaji zaidi!? Mfano wangu wa TANAPA, hawadhani kuwa kuiongeza lugha ya Kiswahili katika wavuti yao ni kuongeza wigo wa kujitangaza!? Taasisi nyingine za Serikali, hazidhani kuwa kwa kutokuwa na lugha ya Kiswahili katika wavuti zao ni kuwanyima baadhi ya watu haki yao ya kupata taarifa!?
Labda wenzangu mnisaidie, yawezekana mimi nafikiri tofauti na ninyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…