SoC02 Kiingereza kifundishwe katika masomo yote ila somo la Kiswahili katika shule za kata za msingi

SoC02 Kiingereza kifundishwe katika masomo yote ila somo la Kiswahili katika shule za kata za msingi

Stories of Change - 2022 Competition

hanayna

Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
5
Reaction score
1
MABADILIKO KATIKA SHULE ZA MSINGI ZA KATA KUTUMIA LUGHA YA KIINGEREZA Katika dunia ya sasa nchi nyingi watoto na vijana wanaenda shule kujifunza mambo mbalimbali watakayoyaitaji kwa maisha Yao ya baadae, shule ni sehemu ambayo watu hujifunza mambo mengi ambayo huwasaidia katika kuyakabili maisha hata kupata elimu juu ya jambo fulani, tumezoea kasema elimu ni ufunguo wa maisha ikimaanisha elimu Ndio kila kitu katika maisha ya mwanadamu kwani mtu hawezi tatua Tatizo Fulani bila ya elimu juu ya tatizo Hilo.

Wanafunzi wengi wanaosoma katika shule za kata za msingi huathirika pale wanapolazimika kuingia sekondari na kukuta masomo yote hufundishwa kwa lugha ya kiingereza isipokuwa somo la kiswahili pekee na mwalimu nae ulazimika kuongea kiingereza bila ya ujali kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawajui hata hicho kiingereza hawana msingi Imara wa mafunzo tangu walipotoka katika shule zao za msingi wengi hulazimika kuanza kujifunza upya pale waingiapo sekondari kwa kununua kamusi za tafsiri ambazo zinaweza kuwasaidia kujua maana mbalimbali ya maneno Fulani.

Hii huwarudisha watoto/wanafunzi nyuma katika maendeleo ya kusonga mbele Kimasomo, huo mda wa kuweza kutafuta maana mbalimbali ya maneno wangeweza kujifunza/kujisomea na kukokotoa maswali ambayo yako katika vidato vyao wanavyosoma, tunaona katika nchi mbalimbali za afrika utumiaji wa lugha ya kiingereza mashuleni katika masomo ya shule za msingi au vyuo vikuu unekuwa umekuwa ni kiitikio kikubwa katika nchi nyingi mfano uganda, Rwanda, Congo, na kenya wao pia ni wazungumzaji wazuri wa lugha ya kiswahili ila katika shule zao wanatumia lugha ya kiingereza kama lugha ya kufundishia katika shule zao.

Hii hupelekea wanafunzi kuweza kuwa na uelewa mzuri pale afikapo katika elimu ya sekondari anakuwa hufahamu vitu vingi kwa maana zake pale mwalimu anapofundisha inakuwa na tofauti na mwanafunzi ambaye kasoma shule ya msingi masomo yake yote katika lugha ya kiswahili alafu akifika sekondari aanze kusoma katika lugha ya kiingereza inakuwa ni vigumu sana kuweza kuelewa kwa upesi kwa mwanafunzi huyo, pia hii huweza kusababisha wanafunzi wengi kuweza kukatisha ndoto zao , unakuta mwanafunzi anaujuzi juu ya kitu fulani ila kwa kutokujua kiingereza kunaweza kumsababishia akakosa ujasili na kuweza kukata tamaa. Kusoma kiingereza kwa mwanafunzi katika masomo ya shule za msingi hii humjenga mwanafunzi kifikra kuwa haya tunayoyasoma huku katika katika lugha hii ndio tunayoenda iufundishwa pia sekondari na Chuo kikuu.

Serikali na wazazi wanaweza kuangalia ni kwanini wanafunzi wengi waliosoma katika shule za msingi za kata wanapoingia sekondari wengine hukataa kuendelea na masomo kwasababu wanaona vitu wanavyofundishwa ibawachukua sana mda wao kuweza kuelewa kwa sababu ya kutokukijua kiingereza mapema na kukielewa na wengine unakuta mtoto alikuwa anafanya vizuri katika masoma yake ya shule ya msingi ila alivyoingia sekondari akaanza kuona vitu ni vigumu sababu ya lugha wanayotumia.

Hii inatokea pale wanafunzi kutojengewa msingi bora wa kuweza kujifunza lugha ya kiingereza mapema katika shule zao za awali na msingi na wao wamezoea kusoma somo la kiingereza kama ziada na kiswahili Ndio bora na msingi kwao wanavyokuja kukumbana na kiingereza katika masomo Yao ya sekondari inakuwa ni changamoto kubwa sana kwao kuweza kuelewa.

Katika shule nyingi za kata za sekondari kunakuwa na mrundikano mkubwa wa wanafunzi ambao ata mwalimu itakuwa ni changamoto kwake kuweza kujua ni nani kaelewa na ni nani hajaelewa, kwani walimu nao pia hupata tabu kwa kuweza kumuelewesha mwanafunzi mmojammoja hivyo basi kufundishwa kwa pamoja uelewe usielewe basi ila kwa mwanafunzi wa shule ya kata angeweza kufundishwa kiingereza kwa masomo yake toka awali asingeweza kupata changamoto ya kuelewa katika masomo ya sekondari mfano katika mitihani ya kujielezea wanafunzi wengi maana ya maneno mbalimbali na kuweza kuandika kwa lugha ya kiswahili.

Serikali inapaswa kubadili katiba ya Tanzania kupitia sera ya elimu kuwa vp shule zote za msingi kuweza kuwa na uelewa na kile kinachofundishwa katika madarasa ya sekondari na elimu ya Chuo kikuu , wanafunzi wengi huu Gia sekondari hawajui kiingereza na wanabaki kukakariri vitu wanavyofundishwa badala ya kuweza kuelewa, inawalazimu kukariri kutokana na mrundikano wa mada nyingi zinazoweza kufundishwa na upatikanaji wa kuweza kusoma neno mojamoja unakuwa haupo, hivyo lugha ya kiingereza ni lugha ambayo inatumiwa na watu wengi katika nchi mbalimbali duniani, hivyo inamuweza mtu kuweza kuelewa na kuwasiliana na watu wengi duniani, katika dunia ya sasa vitu vimetengwnezwa na kuchapishwa kwa maandishi ya nn kiingereza mfano dawa za hospitali, vinywali, vipodozi, kompyuta, mashine, vifungashio vya bidhaa mbalimbali vitu vingi vieweza kutengenezwa na kuchapishwa katika lugha ya nn kiingereza.

Mtu anapoweza kukijua kiingereza basi inakuwa ni rahisi kwake kwa kuweza kuelewa kitu Fulani au bidhaa furani sababu vitu vingi huchapishwa kwa kiingereza. Kutokujua kiingereza kwa wanafunzi wengi kunasababisha kutokujiamini kuelezea kitu Fulani kwa n upana zaidi darasani au Kwenye mkutano au kumbi fulani wao wenyewe wamejikatisha tamaa na misemo yao wakisema (sisi sio mabasi ya njano ) ambao ni wanafunzi wa shule za watu binafsi.

Wanafunzi wengi wanaotokea katika shule binafsi za msingi wao wanapoingia sekondari huwa na uelewa mzuri darasani katika masomo Yao wanayofundishwa sababu walishazoea kufundishwa masomo Yao kwa lugha ya kiingereza na wanauelewa wa misamiati mingi, hivyo inawapekea kuendelea vizuri na walimu wao, mwanafunzi liyetoka katika shule ya msingi ya kata anapoweza kuingia sekondari kidato cha kwanza anasoma vitu vingi ni vigeni kwake kwasababu tu vinewekwa katika lugha ya kiingereza.

Hii inampatia mwanafunzi mtazamo kanakwamba Ndio anaanza kusoma katika maisha yake ingawa angeliweza fundishwa tangu shule ya msingi asingeweza kupata tabu za kuanza kujifunza maana na misamiati mingi sana , wao katika shule za msingi wameweza soma soma la kiingereza na sio kiingereza kwa masomo yote isipokuwa Somo okay kiswahili hii haiwezi mjengea mwanafunzi akaweza kuwa na upeo mkubwa wa kujua misamiati ya maneno mbalimbali ya kiingereza kama angeweza fundishwa masomo yake yote kwa lugha ya kiingereza.

Basi angeliweza kuwa na ujasili katika masomo yake na pia Kwenye kujibu maswali darasani na kufanya mitihani kwa usahihi , midahalo mingi katika shule za sekondari huendeshwa katika lugha ya kiingereza na wanafunzi wengi wasiojua kiingereza wakiwa Kwenye midahalo hawawezi wakatoa hoja wala kujibu maswali sababu wanafahamu hawajui kuongea kiingereza na wanakosa kujiamini mbele ya wanafunzi wenzao na walimu wao wakitakiwa kutetea hoja zao.

Hivyo tunaomba Katika kupitia sera ya elimu iwezwe kubadishwa kwa kuweza kutuma lugha ya kiingereza kufundishia katika masomo yote katika shule za kata za msingi isipokuwa somo la kiswahili pekee ili kuweza kuwaandaa wanafunzi mapema kuweza kujua lugha watayoenda kutumia sekondari na Chuo kikuu ili kuepusha upotevu wa maendeleo katika taaluma, unakuta mwanafunzi anakariri masomo badala ya kuelewa ni nini kafundishwa na maana zake, shule zote za msingi zikiweza kufundishwa lugha ya kiingereza basi tutaweza toa utata Kwa wanafunzi wafikapo sekondari na vyuo vikuu watafaulu sana na kufikia ndoto zao.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom