Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
KIINGEREZA SI LUGHA YETU
__________________
Kumbukumbu zinanirudisha zaidi ya miaka 10 nyuma tukiwa kwenye vimbweta vya Tegeta High school na wanangu Mdax, DVd pamoja na kizazi tukikata topic ya colonialism in Africa. Tayari tumeishakula mihogo yetu ya kukaanga na kachumbari nyingi yenye pilipili. Kila mtu anatema madini kutokana na alichokisoma
Leo hii sisi tukiwa na wachungaji wa ajabu wakina Nabii Tito namkumbuka mwamba wa kiscotland David Livingstone aliyetua Kigoma kama ameletwa na mambo ya kidini kumbe yupo kutupeleleza na kutujua waafrika tukoje ili akawape taarifa ndugu zake juu ya utajiri tulio nao Afrika.
Achana na huyu sisi tukiwa tuna wambeya wakina Shilawadu, Carrymastory, umbeyatz na Juma Lokole wakitupa Udaku huyu alivaa nini na jana alikula nini? Ambavyo havitusaidii chochote zaidi ya kutupumbaza Wenzetu kwa Malkia Elizabeth miaka ya 1857 wanamtuma Richard Burton na John Speke kupeleleza na kujua rasilimali zetu tulizobarikiwa kuwa nazo ili wakija wajitwalie kiurahisi na kufaidisha nchi yao.
Tusiende huko sana najua historia siyo nzuri unawaza kutamani turudi kwenye uzao wetu wa zamani wa Zinjanthropus na ukaanza kumkufuru mungu kuwa uzao wako ni wa nyani badala ya Adam na Hawa au Eva. Tukiangalia kutoka zama za mwanzo za mawe hadi tulipofikia za Chuma ndio wababe kutoka ughaibuni wakaja kututembelea. Huwa najiuliza kwanini hawakuja enzi hizo kabla hatujagundua hata moto? Ndio Mlimwengu mimi ningeamini kuwa wametusaidia kustaarabika.
Nikakumbuka maneno ya wahenga kuwa Mimba ya mwanaharamu huingia mara ya kwanza ila ya pili ni kuwa kakusudia. Kwa hili la kubeza watu wasiojua Kiingereza vizuri tumedhamiria. Sikatai nguvu ya huyu Malkia Elizabeth ulimwenguni ndio maana baaada ya kutuzalisha wote akapata na watoto akatufungulia group la whatsapp (Commonweath) wote tujijue na ikiwezekana kama tuna shida ya chumvi kupitia group hili anaweza kutusaidia. Kumbuka hilo group hadi USA yumo huwa najiuliza naye sijui anataka child support au ndio lazima utulie kisa wenzio wametangulia kuona jua kabla yako. Sijui na hili sakata la Iran naye ataenda kushtaki kwa Bi Elizabeth. Tuachane na hayo ya Iran turudi kwenye mada yetu.
Mlimwengu mimi kilichonipelekea hadi kukumbuka ambayo sikutaka kuyakumbuka ni juu ya hii lugha ya malkia. Tumekuwa tunaihusudu sana maana wengine huitambua kama lugha ya biashara, nembo ya usomi au lugha ya mamlaka. Ila kwetu nahisi tumeizidi kuipamba sana kwa kuita majina mbalimbali kama ngeli,gego, un'gen'ge, kutema yai na kuongezea kuwa ililetwa na meli.
Huku kwetu naona kama tumekuwa washamba sana wa hii lugha. Hii lugha asilimia kubwa ya watanzania ni ya tatu maana tunaanza na lugha ya kikabila kama lugha mama halafu inafuatia kiswahili na ndio tunajifunza Kiingereza. Watu wengi ikitokea ukakosea kuzungumza hii lugha kwa makosa kidogo utachekwa sana na kukufanya kibonzo wakati hii si lugha yetu. Tuliona marehemu Kanumba alivyoenda nje kutuwakilisha baada ya kumpongeza wote tulimcheka kwa lugha ambayo siyo ya kwake.
Tunasahau kwamba licha ya waingereza wenyewe kuwa lugha yao lakini huwa wanachapia. Tunashindwa kujifunza kutoka kwa wachina au wahindi ambao tupo nao nchini wao huzungumza kile wanachokijua ilimradi tu muelewane kwa sababu wanajua siyo lugha yao mama.
Jana imekuwa gumzo baada ya waziri mmoja kukosea maneno machache ingawa alieleweka ikapelekea kuwa mada katika makundi mbalimbali. Namnukuu Prof. Mujwahuki katika majadiliano ya matumizi ya lugha ya kiingereza alisema hivi " Kiingereza siyo tu kukijua intellectually, ni kukitumia katika maisha ya kila siku na ukaeleweka, ukauza unachotaka kuuza,ukaburudisha watu, ukaelimisha na ukashawishi, n.k". na Kukazia kuwa "watanzania tuna tatizo kubwa , licha ya kuchekana kwa wale tunaoona hawakiongei vizuri wengine bado tumejificha nyuma hatutaki kujifunza".
Kupitia nukuu hiyo naweza kusema kuwa hata tunaocheka hatukijui vizuri na wala hatuko tayari kujifunza. Kingine naona masalia ya ukoloni yametuathiri tukiamini kutojua lugha ya malkia ni kama suala la ajabu. Lazima tujivunie na sisi lugha yetu. Tunegechekana kwenye kiswahili ingekuwa vizuri na sasa hivi ni muda muafaka wa kusambaza lugha yetu adhimu ya kiswahili ulimwenguni kote.
Nakumbuka mwalimu wangu wa Kiingereza shule ya Msingi Mwl Mudrikati Sued. Alitusisitiza tusiwe na aibu na wala tusiogope kuzungumza kwa kutumia ushairi huu.
"Kiingereza si lelemama
Wala si lugha ya mama
Kujifunza ni lazima
Ili upate kitu kizima"
Hii imekuwa kama lugha ya ajabu kuizungumza lazima uwe na nidhamu ya hali ya juu, wengine huenda mbali mpaka atumie kilevi ili atoe hofu ndio aweze kutiririka. Vyuoni wakati wa presentation wengine walianza kunywa pombe kwanza ili kupata ujasiri wa kutiririka mbele ya kadamnasi. Hapa ndio huwa nampa pongezi Rais wetu wakija wageni anaamua kuzungumza lugha yetu akiachia wakalima ni wafanye kazi yao. Aache kufikiria namna ya kuwapeleka watanzania kwenye nchi ya asali na maziwa aanze kufikiria misamiati sijui na grammar.
Mlimwengu mimi ngoja niishie hapa lakini tusiendelee kutesana kisa hii lugha. Imefikia kipindi watu wanakosa kazi kisa hawajui kuzungumza kiingereza vizuri wkati wachina hawajui lugha yeyote ila ndio wanaotutengenezea miundombinu yetu. Jamani kazi tunazotaka kufanya hazifanywi kwa kiingereza zinahitaji tu ufanisi wetu. Nimekumbuka zamani tukiwa sekondari kuna rafiki yetu alikuwa anagombea kuwa kiranja wa chalula. Sasa alivyofika kwenye interview akaulizwa kwa kiingereza alichowajibu akasema " English is no but work is forward ever. Waliishia kumcheka na uongozi hakupewa lakini alikuwa na nia na dhamira ya dhati ya kuongoza.
Hii lugha siyo yetu ni ya watu hata wenyewe wanakosea je sisi ni wakina nani tuipatie vizuri?
Imeandikwa na
Mohamed. I. Rwabukoba
Email: mohammedismail613@gmail.com
0762070361
08/01/2020
www.jamiiforums.com
Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?
Hapa Waziri wa Elimu, Profesa Ndalichako akitoa maagizo ya kukamatwa Mhandisi Mchina. KWA WASIOSIKIA VIZURI AMESEMA ‘’Advance payment ya hi nanii milioni mia moja hamsini ,your going to stay on the cell until you provide serious explanation on matter ,because now you cannot play with the...