Kiinua mgongo nssf, ikoje hii?

kisute

Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
54
Reaction score
3
Wana janvi, naomba msaada wenu hapa. Malipo yatolewayo na NSSF kama kiinua mgongo baada ya kutimiza miaka 15 na zaidi ya uanachama hutolewaje? Je, Mwanachama huchukua malimbikizo yake yote kwa pamoja? Mfano; nimechangia Tshs 40,000,000 hadi sasa ndani ya miaka 16. Nimeacha kazi au kuachishwa nitalipwaje?
Nitalipwa fedha hiyo taslim then kiinua mgongo au inakuwaje? Msaada tafadhali kwa waelewa. Nawakilisha.
 
Unatakiwa uwe umechangia kwa miaka 15, then uwe umetimiza umri wa kustaafu (yaani miaka 55 kwa hiari na miaka 60 kwa lazima)! Hata hivyo endapo umeanza kazi kabla ya Julai 1998 michango ilikuwa haihesabiki kama credit moja ya uchangiaji kama ilivyokuja kuhesabika baada ya hapo (kuna fomula ya kufanya convertion-wasiliana na NSSF kwa hili)! Pia kama umeacha kazi kazi kabla ya umri wa kustaafu na umechangia michango kwa miaka 15 au azidi utalipwa Special lump sum ambayo inakokotolewa kwa kuangalia mchango wa mwisho ukizidishwa na idadi ya michango. Ushauri wangu ni kwamba kama umebakisha muda mfupi kufikisha miaka 55 tafuta pa kujishikiza ili uendelee kuchangia ili mwisho wa siku uwe pensionable! Wishing you all the best!
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako.
Je ikiwa bado hujafikisha miaka hamsini inakuwaje?
 
 
Je interest hiyo ni % ngapi? Let's assume umechangia kwa miaka 10 kamilifu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…