Kijana akiri kushirikiana na wenzake kuteka na kuua watoto kisha miili yao kupelekwa Dar

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kwenye video hii kuna kijana anakiri yeye na wenzake kushirikiana kuiba watoto, ambapo kwa kila mtoto wanayeiba hupewa Tsh. 5,000.

Watoto hao huuliwa na kisha miili yao kupelekwa Dar. Video haielezei zaidi kama ni mambo ya ushirikina au nini.

Pia soma: Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”

Video inazunguka sana huko Whatsapp, hii sehemu ametaja Wakuu ni wapi kwa hapa Tz?

Angalia hapa

Your browser is not able to display this video.
 
Dah umaskini ni Laana😩😭 wanashiriki kuuwa watoto kwa malipo ya Tsh. 5,000

Innalillahi wainna ilaihi rajiun.
 
Hapo ni kafara za uchaguzi zinatafutwa wenye kulaumiwa ni viongozi wa CCM wanaosaka madaraka.
 
Usalama wa nchi upo Chini sana
Muda mwingi vyombo vya ulinzi na usalama vinapoteza muda kwenye kulinda chama tawala ,na sio ustawi wa jamii lasima hayo yawepo!wakualumiwa ni wananchi ,nao wamekaa kimya tu,bora hata hao wa simiyu juzi wamepaza sauti.
 
Sidhani Kama Kuna ukweli. Siyo kwamba hii imetengenezwa ili kubadili uelekeo wa upepo????
 
Polisi wametoa taarifa kuhusu video hiyo, wanasema walifika hilo eneo tajwa, na kuwakamata hao jamaa wanaomuhoji huyo kijana na huyo kijana pia na wote aliowataja, viongozi wa eneo husika wamekanusha matukio aliyataja huyo kijana, polisi wanadai pengine alikuwa anatoa hayo maelezo kujinasua na adhabu....wote wapo mikononi kwa Polisi wanaendelea na uchunguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…