Kijana anayechunga mifugo akutwa amefariki na majeraha usoni.

Kijana anayechunga mifugo akutwa amefariki na majeraha usoni.

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Mchungaji akutwa amefariki na majeraha usoni.

1731929177266.jpg

Aron Daniel (16), mkazi wa mtaa wa Msimamo, Kata ya Kihonda, Manispaa ya Morogoro amekutwa amefariki dunia katika eneo la 'Youth Mission' huku mwili wake ukiwa na majeraha usoni.

Baba mdogo wa marehemu, Baraka Kamele, amesema Aron alikuwa akijihusisha na uchungaji
wa mbuzi, ambapo Novemba 16, aliondoka na wanyama hao kwenda machungani, lakini jioni mbuzi hao walirudi nyumbani wenyewe bila mchungaji.

Ameongeza kuwa familia ilianza kumtafuta siku mbili zilizopita na hatimaye jana Novemba 17, mwili wake ulipatikana baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.
 
Mnajua kabisa kuna mchungaji wa waumini na mchungaji wa wanyama, si ungeandika mchunga mbuzi ili ueleweke vema bila utata? Mi nilidhani ni mchungaji wa waumini, nilitaka kushangaa mchungaji gani ana miaka 16 kumbe ni mchungaji wa mbuzi
 
Mleta mada mbuzi kwelikweli, yaani unatuambia mchungaji nikajua wa kondoo wa Bwana kumbe.....
 
Back
Top Bottom