Kijana anayetaka kuwa kiongozi bora huko baadae, atakuwa na tabia zifuatazo

Kijana anayetaka kuwa kiongozi bora huko baadae, atakuwa na tabia zifuatazo

z12f

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
704
Reaction score
572
Kijana anayetaka kuwa kiongozi bora huko baadae, atakua na tabia zifuatazo:

1) Haki itashamiri. Watu wote wa makabila yote na dini zote watashamiri.

2) Cylinder zote za engine ya kiuchumi zitafanya kazi vizuri. Kilimo, misitu, mazingira, uvuvi, utalii, mifugo, biashara, viwanda, madini, nishati, gesi na mafuta etc.

3) Watanzania wengi sana watakua na elimu nzuri ya msingi, zaidi ya nusu ya watanzania watakua na elimu nzuri ya form six.

4) Mikoa yote na makundi yote yatapiga hatua nzuri za kimaendeleo na kimaisha. Hatachukia jamii yoyote, mkoa wowote au dini yoyote.

5) Atajenga miundo mbinu yenye tija na isio na gharama kubwa sana. Runways za viwanja vya kimataifa vya ndege zitakua between 3.3 kms and 4.4 kms. Atajenga barabara ya kiwango cha lami itakayo unganisha Karatu na Mwadui moja kwa moja kupitia kaskazini mwa ziwa Eyasi. Atajenga barabara ya kiwango cha lami itakayo unganisha Lindi na Morogoro moja kwa moja kupitia Mbuga ya Selous. Atajenga kiwanja cha ndege karibia na Songosongo ili kikuze utalii wa Selous na uwekezaji kwenye gesi. Atajenga bandari Rukwa kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika.


6) Atatetea ustawi wa Tanzania kwenye nyanja za kimataifa na atakua na mahusiano mazuri na majirani wema wa Tanzania.

7) Ataiondoa Tanzania kutoka kwenye mahusiano tegemezi ya kisiasa na kiuchumi. Atatetea national sovereignty and self-determination na ataiondoa Tanzania kutoka kwenye makucha ya madeni ya nje hususan madeni ya kibiashara yenye riba kubwa.

8) Atachukia na kupiga vita corruption na ata promote good governance, human rights na ataheshimu legitimate private property rights. Ataheshimu pia tax payers’ and community property rights (matumizi mazuri ya kodi na rasilimali za jamii).

9) Ataweka katiba ambayo Rais hatakua na uwezo wa kulivunja bunge kabla ya uhai wa miaka mitano ya bunge kuisha. Bunge nalo halitakua na uwezo wa kumfukuza Rais. Ikitokea mvutano kati ya hao wawili basi popular referendum ya wananchi itaamua yupi aachie ngazi. Na atakae baki atatawala mpaka hio miaka yake mitano iishe. Ataheshimu uhuru wa mahakama. Ataheshimu na kuimarisha na kuboresha decentralisation na serikali za mitaa. Mapato ya halmashauri za wilaya yatakusanywa na TRA.

10) Atambue kwamba baada ya 2030 AD, huenda tunaishi kwenye siku za mwisho wa dunia. Ingawa hatujui dunia itaisha lini.

Hizi ni tabia (characteristics), na sio utabiri.

Kuna terminologies ambazo ni rahisi sana kuziandika kwa kiingereza kuliko kiswahili. Ndio maana na changanya lugha.

Jamii forums is an informal setting. Ingekuwa a formal setting, ndio nisinge changanya lugha.

Any way, kiswahili chenyewe kina maneno mengi ya kiarabu.
 
Namba 1 hadi 4 ni utabiri au ndo tabia za kijana? Na mimi nasemaje, kijana anayetaka kuja kuwa kiongozi mbovu ni mwenye uandishi kama huu wako.
 
Hizi ni tabia (characteristics), na sio utabiri.

Kuna terminologies ambazo ni rahisi sana kuziandika kwa kiingereza kuliko kiswahili. Any way, kiswahili chenyewe kina maneno mengi ya kiarabu.
 
Back
Top Bottom