Kijana badilika uaminifu wako ndo mtaji wako

Kijana badilika uaminifu wako ndo mtaji wako

Gluk

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
1,859
Reaction score
3,008
Habari wanaJF nikiangalia muda huu ni saa tano kasoro ila nimemua kuandika walaka huu ili kutukumbusha vijana kuhusu uaminifu sehemu zinazotupatia riziki.
Nimeamua kuandika JF nikiamini kuwa itakuwa funzo kwa wengine pia mhusika ujumbe utamfikia kwa urahisi zaidi nikiamini kuwa atausoma pia.
Binafsi nimesaidiwa sana na ninaowajua na nisio wajua na wengine pia wakiwa wanaJF ambao tumekutana humu, na tumekuwa tukishirikiana katika mambo tofauti zikiwemo biashara za kujiingizia kipato..
Miezi kadhaa iliyopita niliwahi kuleta bandiko nikihitaji kijana wa kuuza duka langu la mahitaji ya nyumbani ila wakati nikiendelea na mchakato huo nikakumbuka kuwa kuna member mmoja ambaye tunafahamiana kwa muda mrefu kidogo (ni dogo sana) kwa muda ambao tulifahamiana ni kijana niliyetokea kumuamini sana kuliko kijana yeyote niliyewahi kufanya nae kazi.
Kutokana na hali yake ya maisha ilivyokuwa nikakumbuka kuwa hata mm nilikuwa na hali mbaya kuliko hata yeye ila nilinyanyuliwa na nisiowajua na kufikia hapa.
Nikamfanya kuwa mdogo wangu nikimsaidia katika hari zote na kuamua kumpangia chumba kabsa ili aanze maisha na kumuachia biashara yangu ya duka kwa makubaliano kuwa nitakuwa nikimpa 50%ya anachokiingiza.

Alianza kwa kuwa na nidhamu na pesa na kuniheshimu sana na biashara ilienda vizur sana.
Biashara ikakua ila ghafla akabadilika na kuanza kubadili wanawake kama nguo hapo ndo picha la kihindi lilipoanzia..

Anabadilisha simu na kudanganya kahongwa.
Mara chuma ulete wameiba pesa
Muda wote yuko online Whatsp
Anaongea na simu na kuchati masaa 24.
Kufungua badala ya 1 asubuhi akaanza kufungua saa 3
Nilikuja kugundua kuwa dogo ananichapa baada ya kuja na Id mpya Jf akiomba msaada wa kutumia mobile bank ndo kugundua kuwa dogo anapitisha pesa mlango wa nyuma..
Hii Id yake mpya niliigundua baada ya kushika simu yake akiwa amelala na kusahau kulog out..
Maamuzi niliyoyachukua ni kuuza duka jambo ambalo nimelifanya tiyari maana sina msimamizi.
Pili kesho asubuhi namkabidhi mwenye nyumba chumba chake na kumfukuza rasmi ili aendelee na maisha yake...

Funzo. haya maisha kuna muda mwingine huruma haipaswi kuzidi sana .

NB. Kama kama kuna member yeyote kaja hapa dar hana pa kulala au hana chumba nitampa bure hicho chumba akae bure mpaka kodi itakapoisha..
 
We jamaa mpole sana ndomana wanakupiga, mtu anakurudisha nyuma na kukupotezea malengo unamlea?? Unless hakukutia hasara
Siwezi kumpiga asije nifia bure na simu zote simpokonyi maana ndo atakazouza ili apange chumba na kuanza maisha tena.
 
Ndio maisha kaka, atapata somo na baadae atajuta kwa nafasi yake, wewe ulipomfikisha panatosha.

Next time uwe unaweka watoto wa kike, wale hawanaga mambo mengi sana na ni simple kuwa control, mtazamo tu
 
We jamaa mpole sana ndomana wanakupiga, mtu anakurudisha nyuma na kukupotezea malengo unamlea?? Unless hakukutia hasara
Mkuu kuna mambo mengine yanatia sana uchungu ukiyawaza ila nahisi adhabu ya kumfukuza inamtosha kwa sasa atajifunza maana ya uaminifu katika maisha.
 
We hujaanza kumfundisha mkuu, wala hajifunzi ng'o. Sometimes dawa ya moto ni moto
Mkuu kuna mambo mengine yanatia sana uchungu ukiyawaza ila nahisi adhabu ya kumfukuza inamtosha kwa sasa atajifunza maana ya uaminifu katika maisha.
 
Ndio maisha kaka, atapata somo na baadae atajuta kwa nafasi yake, wewe ulipomfikisha panatosha.

Next time uwe unaweka watoto wa kike, wale hawanaga mambo mengi sana na ni simple kuwa control, mtazamo tu
Watoto wa kike ni sawa ila kwa baadhi ya kazi ni ngumu kwa upande wao.
 
Mkuu pole kwa yote yaliyokukuta ila ndo changamoto zetu vijana ila walio teyar elimika na kuyajua maisha wanajua nn cha kufanya
 
Dogo bwege kweli..utajuta kuchezea shilling chooni

Ila nimecheka sana hapo kwenye kuhongwa na usawa huu wa jiwe
 
Ndo aina ya wadogo zetu tulionao.
Dogo bwege kweli..utajuta kuchezea shilling chooni

Ila nimecheka sana hapo kwenye kuhongwa na usawa huu wa jiwe
 
maisha ya leo ni tofaut na miaka ya nyuma, zaman ukiwa mjanja mjanja ndio unatoboa maana weng ni mambumbumbu, sikuhz ukileta ujanja ujanja ktk kutoboa unaonekana boya na inakula kwako sbb karbn kila yule n mjanja ila haoni ni ujanja kutumia ujanja ujanja kutoboa.
Weng wamekimbilia kwenye udalali(si maanish madalali wote wapo hv), ni uzi mwembamba sana unaomtenganisha mjanja mjanja na tapeli/mwizi n.k
ukitumia ujanja ujanja half unayemjanjia akakusoma, ujue sasa huyo ndio mjanja na ujanja wake anautumia vzr.
Jitahd tu unielewe ni aina gan ya ujanja ni namaanisha, haina ubish maisha ya leo bila ujanja utapata shida, suala lipo kwenye matumizi ya ujanja, kwaio usijeukajisifia kwa umbumbumbu pia.
 
Back
Top Bottom