STUDY NAMI
Member
- Jul 20, 2021
- 7
- 10
Habari mpendwa msomaji wa kiunzi hiki...
Ni kauli iliyojengeka inayosema kwamba "Maisha ni mafupi acha nile ujana" hususani kwa vijana ambao ni chipukizi wakiwa kati ya umri wa kuanzia miaka 20 hadi 30.
Lakini majuto huwapata pale wanapotimiza miaka 30 na kuendelea na kujikuta hakuna jambo la maana walilolifanya toka kuzaliwa kwao licha ya kuwa walibahatika kupata elimu msingi na hata wengine kufanikiwa kufikia ngazi ya elimu ya juu na kutunukiwa shahada mbalimbali na hata pengine shahada ya uzamivu.
Kwa maana hiyo basi ukatika vijana hawa wanajikuta wakiwa kwenye majuto makubwa na kuanza kujilaumu na pengine kuwalaumu watu wao wa karibu waliojituma na kuweza kuyafikia malengo yao kwa kudhani wao walihusika kuwaloga ili nao wasifanikiwe, kitu ambacho si kweli.
Bali ni dhana potovu ambayo watu wengi wasio na mafanikio hupenda kuitumia kwa kigezo cha kujisafisha huku wakisahau muda walikua nao wakauchezea kwa kusema maisha ni mafupi, na hapo ndipo wanapata kujua majuto ni mjukuu.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba vijana hawa wanapoona maisha yanawaendea kinyume na matarajio yao, wengi huwa wanajikuta wakijiingiza katika makundi mabaya na hatarishi yakiwepo makundi ya:
*Watumiaji wa madawa ya kulevya,
* Unywaji wa pombe kupindukia, na
Makundi mengine mabaya zaidi ya biashara haramu ya ngono.
Haya yote ni kutokana na kijana kukosa uthibiti wa maamuzi binafsi na pia Kukosa hofu ya Mungu baada ya kujikuta wapo katika wakati ambao hawakutarajia katika historia ya maisha yao.
Ukiacha tatizo la baadhi ya vijana kuchezea ujana wao, pia mtu yeyote anaweza kujikuta akiwa katika kipindi ambacho hakukitarajia kutokana na mabadiliko ya
Wizi, unyang'anyi kwa kutumia silaha, ujangili na mengine mengi.
Licha ya kuangazia jambo hili la mtu kukumbana na mabadiliko hasi bado waathirika wakubwa ni vijana kwani wengi wao hawapendi kuomba msaada wa kushauriwa kutoka kwa wakubwa wao wakiwepo Wazee, Baba, kaka, Dada au walezi kwani sio wawazi kuelezea masaibu yanayo wakumba badala yake mhanga hupenda kufanya maamuzi magumu.
USHAURI NI MUHIMU
Kijana anaweza kupatiwa Ushauri na Elimu ya maisha ambayo Mara nyingi hawezi kuipata shuleni, na hivyo kuweza kuyafikia mafanikio kikamilifu.
UJANA NI DHAHABU
Jambo la msingi ambalo vijana wengi wanalisahau ni kutambua kuwa " Ujana ni dhahabu". Hivyo ili dhahabu iweze kung'aa inapaswa ipitie kwenye Moto mkali, vivyo hivyo kwa kijana yampasa kufahamu ili aweze kung'aa kesho anapaswa apambane katika kujishughulisha na kazi halali pamoja na kutilia bidii na umakini, ilimradi iwe halali hata kama hana taaluma nayo, lakini awe tayari kujifunza ndani yake, Hapo lazima afikie malengo makubwa na kupata mafanikio.
Kwa kufanya
Hivyo kila kijana akijiamini na kuchapa kazi, hatutaona watu wanaochanganyikiwa kwa ugumu wa maisha wala hatutasikia tena neno " Hakuna ajira".
MWISHO
Tujitahidi kuchunguza mienendo ya vijana wengi katika familia zetu na jamii nzima ili kuwatia moyo vijana na kuwapa ushauri wasije wakakata tamaa wakaishia njiani.
Jamani naombeni kura zenu wadau, kwani kura yako inaweza kubadilisha maisha yangu na yako pia. Kwasababu kusudi langu kwako haliwezi kutimia bila ushirikiano wako.
Asante

- kimazingira. Mfano; Mafuriko na ukame.
- kiuchumi. Mfano; Kupoteza kazi
- kifamilia. Mfano; Mgogoro kwenye mahusiano
- kijamii. Mfano; Vita vya wafugaji na wakulima
- kitaifa. Mfano; Vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Upvote
1