SoC02 Kijana jivunie kile unachokifanya uweze kufikia ndoto zako

SoC02 Kijana jivunie kile unachokifanya uweze kufikia ndoto zako

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 26, 2022
Posts
14
Reaction score
10
Ni wakati vijana kujivunia kile wanachokifanya. Kazi iwe ndogo au kubwa ukiifanya kwa kujivunia unaweza kufikia ndoto zako.

Ni kweli kwamba vijana hasa waliohitimu elimu ya juu (tertiary education) wanajikuta wakiwa wanyonge hasa baada ya kujikuta nje ya matarajio yao yaliyotokana na taaluma walizozisoma. Ni wakati vijana wa namna hii kujishugulisha kulingana na fursa iliyopo na kutumia fursa hiyo hiyo kutimiza ndoto zao.

Mfano ni mimi mwenyewe baada ya kuhitimu shahada ya kwanza ya Sera na Miradi katika Elimu (OUT, 2015) nilijikuta katika lindi la mning'inio wa msongo wa mawazo baada ya kusubiri ajira kwa miaka 4. Lakini taratibu niliweza kubadili saikolojia yangu kwa kujihusisha na fursa tofauti.

Katika fursa zote, nilijikita zaidi katika ufugaji wa kuku. Jinsi nilivyoanza:

Kwanza nilianza na kuku wa kienyeji 8 ambapo nilinunua mitetea 7 na jogoo mmoja (mbegu kubwa). Baada ya mwaka mmoja nilijikuta na kuku 180. Baada ya mwaka niliuza kuku 130 na kupata Tsh 1,400,000. Hela hii nilitanua wigo wa ufugaji kwa kujenga mabanda ya gharama nafuu na kuanza ufugaji wa broillers mia 2.

Hivi sasa najivunia kazi ya ufugaji ingawa pia najishughulisha na kazi za tarjama (translation) na uhariri (editing).


Ufugaji umenipa mafanikio mengi hasa:

1. Kuwa sawia kisailolojia​
2. Kununua shamba na kiwanja​
3. Kuwahudumia vema familia​
4. Kupanua uelewa wa masuala ya ufugaji nje ya taaluma yangu​
5. Kupanua mtandao wa marafiki.​
6. Kujua zaidi kuhusu haki za wanyama.​
7. Kupata burudani. Mifugo hukuburudisha pindi unapoitazama na hukupa wasaa wa kuzungumza na nafsi yako.​

USIWE MNYONGE NA KAZI YAKO. IFURAHIE NA UIFANYE KWA UKUBWA.

"Ukishindwa kufanya jambo kubwa basi fanya jambo dogo katika hali ya ukubwa."___Plato
 
Upvote 1
Back
Top Bottom