hafidhasha
Member
- Jul 24, 2021
- 18
- 19
Kwa jina naitwa Marina, ni kijana mwenye miaka 30, mzaliwa na mkaazi wa Zanzibar.
Nimemaliza elimu yangu ya chuo kikuu nchini China mwaka 2020, ambapo nilisomea udaktari wa binaadam, na nimefanyia mafunzo yangu ya vitendo ( internship ) Bugando Medical Center iliyopo jijini Mwanza.
Kama inavyojulikana kusomea udaktari ni kazi kubwa Sana, ni wito na inataka maandalizi makubwa Kwa moyo na akili, haikua Safari rahisi kwangu, nilikutana na misukosuko mingi kusoma katika nchi ngeni, kuna wakati nilitaka hata kukata tamaa niache kusoma nirudi nyumbani lakini nilizungukwa na marafiki walionisaidia kuweza kuendelea na masomo, na msaada pia kutoka Kwa wazazi na ndugu wa karibu, lakini kusomea udaktari tena nje ya nchi ina athari Kwa akili na mwili na inataka jitihada ya ziada.
Nashukuru mungu nilimaliza masomo yangu salama na nikarudi nyumbani na degree yangu ya udaktari.
Wakati nipo nyumbani kabla sijaanza mafunzo ya vitendo, Baba angu aliniambia “chuo wamewafundisha Mambo mengi Sana ya muhimu, lakini hawajawafundisha jinsi ya kutumia ulichojifunza na kipaji ulichonacho kutengeneza pesa, na vijana wengi wanasoma kwa bidii Sana Kwa kutegemea kuajiriwa, hawana fikra ya kwamba kitu cha muhimu zaidi Kwao baada ya chuo ni kujiajiri, ni kufanya utafiti uwezo wao ulipo, vipaji walivyo navyo na jinsi gani wataingiza pesa kupitia vipaji hivyo.
Hivyo mwanangu, tafakari vipaji vyako na jinsi gani utavitumia kukuingizia kipato, kwani ajira sio kitu tunu, usipoteze muda wako kusubiri ajira wakati unaweza kuanza kujiajiri mwenyewe, ajira ikija imekuja, haijaja unaendelea na Mambo yako” hapo nikajifkiria na nikaamua kuanzisha biashara ya urembo asili, mafuta ya nywele na mwili, na nilianza nikiwa na mtaji wa 30,000 tu.
Mwanzo haikua rahisi kutafuta wateja na kutangaza biashara yangu, na bidhaa zilikaa kwa mda mrefu Sana bila kununuliwa Ila sikukata tamaa. Baada ya miezi kadhaa nikaanza mafunzo yangu ya vitendo mwanza, nilipofika mwanza niliendelea na internship yangu huku nikiendelea kutangaza biashara yangu na nilibahatika kupata wateja wa kutosha kwani nilikua naenda kwenye saloon na supermarkets kutangaza bidhaa zangu, wapo wengi waliozikataa Ila wachache walioikubali biashara yangu walisaidia Kwa asilimia kubwa maendeleo ya biashara yangu.
Baada ya mwaka mmoja nilimaliza internship na kurudi nyumbani Zanzibar, nilifanikiwa kupata wakala mmoja mwanza ambae alichukua bidhaa kwangu Kwa jumla yeye akauze Kwa reja reja.
Baada ya miezi mitatu nilienda kufanya mtihani wa MCT Kwa ajili ya kupata leseni ya udaktari lakini sikufanikiwa, na hakuna anaetaka kuajiri daktari asie na leseni, sio bara wala sio Zanzibar, hivyo lililobaki ni kukaa nyumbani Kwa miezi zaidi ya sita bila ajira na kusubiri mtihani mwengine mwisho wa mwaka ambapo pia nikifeli tena nisubiri miezi mengine tena Kwa ajili ya mtihani mwengine, na baada ya kufeli mara tatu unatakiwa urudie tena internship, hivyo ni mzunguko usiojulikana mwisho wake, na ni kitu ambacho kinaweza kukatisha mtu tamaa ya kuendelea, na Hali ya maisha ilivyo ningekua na msongo wa mawazo zaidi kama ningekua sijishuhulishi na biashara yangu binafsi.
Nikiwa nasubiri mtihani mwengine huku nikijishuhulisha na biashara yangu nimepata fursa ya kuchaguliwa katika kundi la vijana kugombania tunzo nikiwa katika category ya young entrepreneur of the year female, ni fursa kubwa kwangu kwani napata kukutana na watu tofauti ambao wananifunza na wananiamsha akili, na napata kuongeza connections, hata nisipopata tunzo fursa pekee ni zawadi tosha, kwani nisingekutana na niliokutana nao sehemu Nyengine, wala nisingejifunza niliyojifunza.
Kama nilivyosema mwanzo nilianza biashara yangu na mtaji wa 30,000 TSH tu, Kwa sasa nashkuru Mungu naingiza mpaka 500,000 TSH Kwa mwezi kupitia biashara yangu, nna wateja ndani na nje ya Zanzibar, nasambaza bidhaa zangu madukani, maofisini na kwenye supermarkets na Mambo yanaenda vizuri, sina stress za kukosa ajira kwani naingiza pesa japo kuwa si kubwa, na kupitia mda wangu wa kukosa ajira nimepata nafasi ya kuandika, Nina vitabu viwili vilivyokamilika, kimoja cha mashairi ya kiswahili, na chengine cha quotes cha kiengereza, ambavyo vyote natarajia kuchapisha nikijaaliwa kupata connection na muongozo.
Sikukata tamaa wakati nasoma na nikamaliza masomo yangu, wala sikukata tamaa baada ya kufeli mtihani wa leseni, niliweka akilini kwamba sio kila changamoto ni angamizo, changamoto nyengine ni baraka hivyo sikusubiri kuwezeshwa, nilipewa ushauri wa kujitegemea na mzazi wangu na nikaufata, sijawahi kupata msaada wa kifedha kutoka Kwa mtu yeyote Yule katika kukuza biashara yangu, nilipanga malengo yangu na nipo njiani kuyafikia, sijafika nnapopataka Ila mwaka huu ni tofauti Sana na mwaka Jana, nilianza na hatua moja na sasa nimefika mbali, ninapochoka na kuanguka sikati tamaa, napumzika, nanyanyuka naendelea na Safari.
Msikate tamaa vijana wenzangu, siku yako itafika Tu hata baada ya miaka mingapi, Mungu hajakuumba kuja kuteseka, ukikumbana na matatizo yeyote ujue ni Mungu anakuandaa na ushindi unaostahili, muamini yeye kwani hukupa unachohitaji Kwa wakati, hachelewi.
Na ukiamua kumuamini yeye, na ukafanya jitihada kupigania malengo yako, basi Mungu atakukutanisha na watu sahihi kwako ambao watarahisisha Safari yako, jioneshe, na dunia itakuona, itakutambua na itakuthamini.
Tafakari, ni kipi kipaji chako na kitakusaidia vipi kuzalisha pesa, muhimu zaidi, kitakusaidia vipi kufanya dunia kuwa nzuri kuliko ulivyoikuta, kitakusaidia vipi kuacha alama yako katika dunia, ili ukifika wakati umeondoka watu wakukumbuke na tabasam usoni mwao.
Ili uwe UMEISHI na sio KUPITA NJIA tu duniani.
Kwenye picha nimeambatanisha bidhaa zangu nnazotengeneza katika picha ya Kwanza, na picha ya pili ni moja ya chapter ya kitabu changu cha quotes.
Ahsante.View attachment 2335881

Upvote
16