Kabila awafuta kazi maafisa wakuu
Imeandikwa na Mwandishi wa BBC.
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo - DRC,
Joseph Kabila amewafuta kazi zaidi ya maafisa 80 wa serikali wanaolaumiwa kwa ufisadi.
Rais Kabila pia ameagiza kustaafishwa kwa zaidi ya wafanyakazi 1,200 ambao amesema wamekuwa wakifanya kazi ilhali wameshatimiza umri wa kustaafu.
Mwandishi wa BBC Lubunga Byaombe anasema wengi wa maafisa waliofutwa kazi ni kutoka wizara za Ardhi, Fedha na ujenzi.
Maafisa hao wanalaumiwa kwa kutekeleza au kuruhusu vitendo vya ulaji rushwa wakati wa utendaji kazi.
Rais huyo wa Congo katika siku za hivi karibuni amekuwa akiendesha kampeni ya kupambana na ulaji rushwa katika serikali yake, na mwezi uliopita aliwafuta kazi mahakimu kadhaa akiwalaumu kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.