Kijana kwanini unaingia kwenye ndoa?

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
NDOA: Ni makubaliano ya muingiliano utakaohusisha hisia,
Muingiliano utakao husisha miili ya watu wawili walioamua kuanzisha Familia ya Baba na Mama..
Kwa maridhiano ya wazazi wao...!
Je ndoa kwani lazima iidhinishwe na mchungaji au sheikh au Askofu?
Hapana sio Lazima.
Kukishakua na maridhiano ya watu waliokubaliana kuishi Kama mume na mke kwa kupenda kwao
Wanaweza kua ni wanandoa kabisa..!
Haya mengine ni nyongeza tu za kimaslahi
Kidini na kisheria..haimanishi bila hayo
Hawa watu hawawezi kua wana ndoa.

SASA

Kijana unataka kuoa kwasababu zipi?

Je ni kwasababu umri umeenda na wenzako wote,wana vyeti vya ndoa toka makanisani mwao,na kwa mkuu wa wilaya?

Je unaoa kwasababu ndugu wamekusema sana?

Unaoa kwasababu ni utaratibu umeukuta basi nawewe huna budi kufuata mkumbo.?

Au unaoa kwasababu mama yako anataka mjukuu wa kupakata?

Au unaoa kwasababu ni muda umefika nawewe uishi?

Unaoa kwasababu unataka nawewe uchangiwe,na kupokea zawadi Kama unavyowatoleaga wengine?

unaoa kwasababu kuna mikataba na vitu vingine lazima ujaze marital status??

Basi kama unaingia kwenye ndoa kwasababu Kama hizo na zifafanazo na hizo basi tambua...
Ndoa sio kwajili yako maana itakushinda

INGIA
Kwenye ndoa kwasababu umependa wewe mwenyewe toka rohoni mwako.

Kiasi kwamba uko tayari kuijaza dunia kwa maongezeko ya uzao..
Na utawala utakaoambatana nao,
Yaani kusiwe na sababu yoyote zaidi ya upendo kati yenu...
Pesa isiwe sababu,
Mali zisiwe sababu...basi mtafurahia.

BINTI

Unaingia kwenye ndoa na huyo mwanaume kwasababu zipi?

:je ni kwasababu marafiki na mashosti zako wote wameolewa,wako kwenye majumba yao...nje wanakuchekea je unajua wanayoyapitia ndani?

: je unaolewa kwasababu unataka uwatambishie wanawake wenzako,kua umefanya party kwenye ndege,kwenye boat?
Umefunga harusi iliyo gharimu mamilion ya fedha?

: Au unaolewa kwasababu kwenu ni hohe hahe,yaani pako pako tu sasa umeamua kuolewa ili huyo bwana umtegemee akafanye mabadiliko kwenu...?
Kwanini mama yako hakukupatia huyo baba tajiri? Kama hio ndio target yako kwenye ndoa?

: unaolewa kwasababu umeshahangaika na wanaume vya kutosha sasa unatafuta mtu wa kukufichia aibu.?

: Au unaolewa ili nawewe upate heshima kua ni mkewa fulani?

KAMA unaolewa kwa sababu hizo na nyingine zifananazo na hizo tambua fika hiyo ndoa,
Hutaiweza utatumika tu ndivyo sivyo.

OLEWA

Kwa sababu umempenda mtu toka moyoni.
Kwasababu umekubali kua msaidizi wa kweli kifikra,kiuchumi,na kijamii kwa huyo mwanaume.

Olewa kwa sababu

umekubali kwa moyo wako wote kua unaenda kumsaidia huyo jamaa kuijaza dunia...maana yake hautakua na sababu ya kumsumbua na kumnyima huyo bwana ngono yake kwakua ni wajibu wenu kupeana.

ELEWA HILI

Huyo unayemuona ni Handsome..kuna siku linaweza kutokea la kutokea uso na umbo likaharibika....lakini hilo halitakuteteresha maana umependa utu wake.

Unaweza kumwoa binti kwa shape yake lakini baada ya kujifungua,umbo lake likabadilika na kuharibika lote...lakini hill likawa halikusumbui tena maana ukipenda utu wake umbo halitazitatanisha hisia zako kwake.

KUNA

Watu waliolewa kwababu
walitaka wawakomoe Ex zao,lakini walikimbia baada ya kuona giza tu huko.

Wako walioolewa kwa sababu zao binafsi...

Lakini walipoenda kukosa watoto walikimbia.
Walipofika na kukutana na maneno ya wifi zao waligeuka.
Wengine walipofika huko walienda kugombanisha watu na mama zao.
Wengine walipofika huko walienda kudhoofisha uchumi wa mwanaume ili kuimarisha uchumi wa nyumbani kwao...
Pasipo kujua kua kwake ni kwa huyo mwanaume...
Na kile anachofanya kwao ni kuingilia majukumu ya baba yake tu.
Ahsante.

Content created by : Creezle Farey
 
Sawa
 
Mm naona ndoa Haina uzoefu na wengi tunabet unaweza kuona ni chema kumbe sio na unachohis sio chema ndo kikawa sahihi
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Uzoefu unaupata vipi wakati upo nje ya field? πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Kuoa na kuolewa ni jaliwa ambalo ni wajibu ambo unapaswa kutimizwa, kuchelewa au kuwahi hakupunguzi uzito wa kutimiza wajibu huo.
 
nani mwalimu wa ndoa?

Anifundishe nami nimwelewe... In bukuku's voice....

Kila la khery kwa waliopo, wanaotarajia na watakaotarajia kuingia kwenye ndoa.....

Good luck πŸ‘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…