Fadhili Paulo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2011
- 3,211
- 993
Kijana mmoja amekutwa akitoa huduma za tiba zinazotolewa na madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika zahanati bubu maarufu kwa jina la kwa Docta Kondoliza eneo la Mji mpya Majohe kinyume na sheria.
Kijana huyo bwana Nathan Wales anayejiita daktari katika eneo hilo la mji mpya Majohe,amekutwa akiendesha shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa huduma asizotakiwa kuzifanya ikiwemo huduma za madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake,kuendesha huduma za duka la dawa kinyume na utaratibu,kutoa huduma za maabara pamoja kukutwa na vifaa mbalimbali ikiwemo vifaa vya kutoleamimba.
Naibu msajili wa hospitali binafsi nchini dakta Mahewa Lusinde,amesema kwa sasa serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii haitakaa kimya kuvumilia watu wenye uchu wa fedha kufungua zahanati bubu kwa malengo ya kupata fedha wakati ni hatari kwa taifa huku mratibu wa usajili wa hospitali binafsi kutoka manispaa ya Ilala Bi Semeni Segella akiomba wananchi kufichua kwa kutoa taarifa za zahanati zote ambazo zinaendeshwa kinyemela.
Mmiliki wa zahanati hiyo bwana nathan wales,alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo kabla ya kufikishwa na maafisa wa wizara ya afya na ustawi wa jamii katika mahakama ya jiji kujibu mashtaka yanayomkabili,alikiri kuendesha huduma hizo tangu mwaka 2010.
:: Kijana Mmoja Amekamatwa Akitoa Huduma Za Tiba Ktk Zahanati Bubu