Kuna watu wengine wana andika article kutokana na mambo yaliyo mkuta yeye na adhani watu wote dunia yamewakuta kama yeye, ukweli ni kwamba kila mwanadamu anakutana na changamoto tofauti katika maisha na hakuna suluhisho moja la changamoto hizo. Ndoa ni muunganiko wa furaha wa watu wawili walio pendana kwa dhati kutoka moyoni mwao. Ndoa haina uhusiano na maisha yako ya ujana kama yalikuwa ya raha au shida bali ni hisia za ndani za moyo wa mtu kwa mwenza wake ambazo hazijali utajiri au umasikini au mazingira ambayo ulioyopitia katika maisha bali ni moyo kuridhia uliye mpenda. Kunatofauti kubwa kati ya ujana na ndoa, ujana unaweza ukawa unatimiza haja zako za mwili na haina maana kwamba ndio kipindi cha furaha zaidi ya kipindi cha ndoa. Hivi ulishawahi kujiuliza ni furaha ya kiasi gani utakayoipata pale utakapo jiona una mke na watoto unaowapenda na watu wanakuheshimu wewe na familia yako? unapo rudi nyumbani watoto wanakuita baba baba baba, mke anakuita mume wangu mpenzi, usiku wakati wowote umemkumbatia mkeo unayempenda, ni furaha isiyo na kipimo. Ujana unawakati wake na furaha na thamani ya ndoa haiwezi kulinganishwa na kitu chochote.