MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hayati Lemutuz alisisitiza sana vijana kumudu kuwa na sehemu anapopaita kwake hata kama amepanga. Hata kama ni chumba kimoja hakikisha unamudu kulipa kodi ya pango. Hiki kiwe kipaumbele cha kwanza kwa kijana wa kiume. Kushindwa kumudu kodi ya pango huja na gharama kubwa inayodhalilisha utu.
Nimeandika huu uzi kwa masikitiko makubwa sana baada ya jamaa yangu mmoja kufunga ndo leo huku tukijiuliza maswali mengi sana ITAKUWAJE? Kiufupi ni kuwa jamaa na huyu mkewe walikuwa wapenzi kwa muda mrefu na mara nyingi huyu manzi alikuwa akidai jamaa ni mwanachama mtiifu wa chama cha mabahili.
Maneno yalienea sana. Wengi tulipuuzia kwa sababu ni lawama za kawaida. Tulishtuka bidada alipoanza kuchepuka na jamaa mwingine anayeishi mji wa mbali kidogo. Madai yake akadai huyu jamaa yetu ana mashine ndogo hamridhishi. Hii ilishtua sana na kusikitisha.
Tukiwa tumebaki na mshangao ndo tukasikia jamaa yetu anaoa huyo mdada mdhalilishaji. Lakini cha kushangaza mchepuko akamfuata mchungaji na kumwambia asithubuti kufungisha hiyo ndoa maana bidada ni mtu wake na tayari kashachomoa mimba yake.
Mchungaji akaona atulie na kusikilizia kwanza. Wakati akisikilizia tukashangazwa kuona jamaa na manzi wake wameamua kufunga ndoa ya bomani. Pigo kuu ni kuwa baada ya ndoa manzi anaenda kuanza chuo mji anaoishi mchepuko wake. Kimsingi ni huzuni.
Baada ya kujiuliza kuwa imekuwaje huyu jamaa yetu kuwa dhaifu kiasi hiki? Tumegundua baba mkwe wake ambaye ni tajiri ndo yuko nyuma ya kila kitu. Baba mkwe anamkubali jamaa kinoma kiasi kwamba kamkabidhi APARTMENT aishi bure eneo la ushuani.