Hashim Muyinga
New Member
- Aug 19, 2022
- 1
- 0
Nasema na kijana, kijana yoyote aliezaliwa katika ardhi takatifu ya Tanzania.Kijana mwenye kuwiwa na mafanikio na mwenye mkururo wa fikra za kimapinduzi na maendeleo. Najua umezaliwa katika mazingira ya Jamii yanayosema soma kwa bidii, ufaulu vyema na upate kazi nzuri na kadhalika.
Tambua ya kwamba tupo katika ulimwengu uliobadilika sana.Ulimwengu ambao unahitaji sana maarifa kuliko kiwango cha Elimu uliyokua nayo.Elimu unayoipata iwe chachu ya kufaham dunia vizuri na kukufungulia milango ya fursa mbali mbali ,kufanya bunifu zinazoweza kukukwamua wewe binafsi na nchi kiuchumi, kubuni njia za kutatua matatizo na magonjwa mbali mbali yanayoikabili jamii yetu kiujumla.
Ondoa mategemeo ya kwamba ukae ofisini ukiwa na suti na tai kutegemea mshahara wa kila mwezi.
Kijana tambua nchi yako pendwa bado inakuhitaji sana kuikomboa kwa kufanya mapinduzi ya kubuni mifumo tofauti ya kibiashara,mifumo tofauti ya kilimo,kubuni madawa tofauti ya kupambana na magonjwa Sugu,kubuni njia za kutatua matatizo mbali mbali yanayoikabili jamii kama Elimu bora na yenye tija, upatikanaji wa maji safi na salama ,kutatua migogoro ya kijamii na n.k.
Tambua ya kwamba tupo katika nchi ambayo licha yakua na maeneo makubwa ya kufanya shughuli za kilimo chakula kimekua kikipatikana kwa shida na kutegemea sana kilimo cha mvua kulisha nchi nzima wakati kunauwezekano mkubwa wa kubuni mifumo ya umwagiliaji kuongeza uzalishaji na pia kutumia mifumo tofauti ya kilimo kama kutumia Greenhouses kulima sehemu ndogo na mazao kuzalishwa kwa wingi ,tunahitaji sana ubunifu wako na mawazo yako ya ukombozi.
Tambua ya kwamba ulimwengu wa sasa hivi umejikita sana kwenye nguvu ya mtandao na Teknolojia na ndipo kasi ya maendeleo ilipo. Haikuhitaji kukaa ofisini ili kukuingizia kipato bali unaweza kutumia platfoam tofauti kufanya biashara na kukusogezea masoko kwenye kiganja chako cha simu na pia kuifikia jamii kwa uharaka,kutumia teknolojia hiyo hiyo kwa kutumia mtandao na kukunufaisha katika masoko ya kigeni ya fedha na kukuingizia kipato.
Mtandao ukawe chachu ya kukuelimisha kifikra,mtazamo na kukukomboa kiuchumi na sio kutumia mitandao kwa mambo yasiyo ya msingi.
Kijana tambua ya kwamba nchi yako pendwa inahitaji sana ubunifu wako kwan bidhaa nyingi na bunifu nyingi zinatoka nchi za nje na kuingia ndani .Tubuni na kutengeneza bidhaa zetu tuache kutegemea bunifu za nje na kuthamini vya kwetu ili tukuze uchumi wetu kama nchi.
Kabla sijamaliza kijana tambua ya kwamba kile kidogo ulichokuanacho huenda ni wazo,ubunifu au talanta tofauti tofauti kama mziki,uchoraji,kuogelea n.k ni mali za adimu ulizobarikiwa nazo na Mungu, tengeneza mazingira ya kuvikuza kwani jamii yetu ya sasa inavitegemea sana.
Katika jamii yako ya sasa inayokuzunguka jitahidi sana kuana nidham kwa watu wanaokuzunguka na vitu unavyovifanya.Jali na thamini sana watu bila ya kujali rika,cheo au mali alizokuanazo na utaona maisha yakibadilika.
Imeandaliwa na,
Hashim Hussein Muyinga
Contact: 0659219194

Upvote
0