bomouwa
JF-Expert Member
- Jun 19, 2014
- 1,149
- 800
Ndugu zangu wa jf habari za muda huu?
Najua sasa ni mfungo na pengine tumekua tunachoka sana maana lazima tushughulike ili tupate chakula chetu cha kila siku wakati dini nayo inatudai kutimiza nguzo muhimu,lakini yote ni sehemu ya maisha na inatupasa kukamilisha kwa mujibu wa imani zetu.
Kama kanuni za bunge zinavosema kwamba kama unataka kuzungumzia jambo ambalo unamaslai nayo basi hunabudi ku declare interest ili ijulikane sasa na mimi nasema katika mada hii nazungumza kupitia elimu mbalimbali za kiujasiria mali na nimeona ni vema nikawaoa hofu vijana wenzangu ili nao waweze angalau kupata mafanikio japo kidogo na wawe na amani ya kweli katika maisha yao.
KWANINI UNAOGOPA KUFUNGUA BIASHARA?
Katika uhalisia uliopo ni jambo lisilopingika kwamba kila kijana anauwezo wa kufungua biashara kwa kua katika biashara mtaji mkubwa ambao binaadamu anao ni "AKILI" yaani ukipata akili ndipo unaweza kufahamu ni kwa jinsi gani utahitaji fedha "financial capital" kwa ajili ya kutekeleza azimio lako.je,hauna akili?
Kwa tafiti isiyo rasmi nimeona vijana wengi sana wanaakili ya kufanya mambo mengi tena ya msingi lakini wanasemaga hawana mtaji.huo ni "UOGA".Kwanini?Kwasababu ubongo hutekeleza jinsi taarifa ilivopelekwa na hivo inangoja utekelezaji wake kutimiza jukumu lake tu.kama unataka biasbhara ya mil10 na kipato chako ni 50elfu maana yake hautaweza kufanikisha kwa kua umewekeza akili yako kama mtaji wa "KUSADIKIKA" na hivo hata ukipata wazo la kuwekeza biashara ya kiasi cha 30elfu tayari akili itakataa kwakua tayari mwanzo ulishaiaminisha huwezi biashara ya mil10 kwakua hauna.
SASA UNATOAJE UOGA WA KUANZA BIASHARA?
kwanza jitambue wewe ni nani(labda mfanyakazi)?unahitaji nini(biashara)?unalengo lipi(kutengeneza faida ya laki2 kwa mwezi)?matarajio yako ni yapi(kupata mtaji wa mil10)?kwa muda gani(miaka5)?
mfano:Wewe ni mfanyakazi pengine kipato chako ni laki1 kwa mwezi kama faida ya mshahara wako,sasa weka nia ya kuanzisha biashara ya 50elfu ili iweze kuzalisha lengo kuu(itengeneze mtaji wa mil10) kwa muda ambao unauhitaji yani malengo yako yawe na TIME BOUND usifanye kwa kubahatisha.kuna biashara nyingi ndogondogo zenye zinazohitaji mitaji midogo ya kifedha ambazo zinaweza zikawa zinaingiza sana faida.
Kama ukijitahidi kufata utaratibu uliojipangia kwa kukusanya faida yako ipasavyo basi amini ndani ya kipindi ulichopanga biashara yako itakua na pia itawezesha kukuanzishia biashara nyingine ambayo ndo ilikua lengo lako kuu.
KWANINI UMEFUNGUA BIASHARA NA HAIENDELEI?
Biashara yako itakua haiendelei kama tu utakua unafanya mambo yafuatayo
-acha anasa za dunia zisizokua na msingi
-kupanga faida kubwa kwa bidhaa ambazo zinatumia muda mrefu kutoka
-lugha ya mawasiliano na wateja kua mbaya yaani poor customer care
-kutokua na usimamizi bora wa biashara yaani improper business management
-matumizi mabaya ya rasilimali za biashara ikiwemo matumizi ya sehemu ya mtaji wako
-kutoweka mabadiliko ya biashara yako kuanzia mwanzo mpaka sasa,namaanisha mteja anatakiwa kuona mabadiliko ya mahali anapopata bidhaa ikiwemo muonekano wa mahali pa biashara ndo maana unakuta wenye biashara za maduka makubwa kila baada ya muda fulani wanabadili settings ingawa bidhaa ni zilezile
-penda kusoma juu ya biashara yako ili uendane na mazingira ya wakati husika
-fahamu kwa undani biashara unayofanya ili uweze kumfanya mteja wako anunue.
NOTE
Katika biashara yako unahitaji sana UMAKINI ili uweze kufanikisha nia yako na pia kila kinachotumika katik biashara nilazima KIANDIKWE ili mwisho wa siku unapofanya evaluation uweze kujua ni kwajinsi gani faida imepatikana na imekosekana.
Ndugu zangu hasa vijana wenzangu,niwaambie tu kua kuna kila haja ya kua na moyo wa UDHUBUTU yaani "DARING HEART" ili uweze kupata ujasiri unahitaji kufanya lile ulilopanga pekee na si vinginevyo maana kuna watu wapo wanakuangalia na yamkini hawataki kukuona ukifanikiwa sasa wanachotaka ni kukushusha ari KUKUDEPRESS ili tu ukate tamaa lakini wewe songa mbele na usirudi nyuma HAKIKA UTAONA MAANA YA ULICHOANZISHA.
Wana jf mimi ni kijana ambapo nkiwa chuo mwaka wa kwanza 2003, mwenzenu nilianza biashara na mtaji wa 75elfu kwakupika chakula na kusambaza katika vyuo ingawa askari walintesa lakini miaka 2 baadae nkatengeneza faida ya 2.7mil ikanifanya nianze kuuza mifuko ya salfet na hii mieusi inajulikana kama mifuko ya kondom,mwanzo nlianza kwa mtaji wa 2.5mil kununua kwa wholesalers nakuiuza rejareja ndani ya nchi hasa mkoa wa dar es salaam katika masoko ya nafaka na maduka ya mitaani mwaka 2006 ikanichukua miaka6 yaani 2012 nikaanza agiza viwandani kenya na china na ninauzia wafanyabiashara wa jumla katika mikoa 13 ya hapa Tanzania(najua wapo watakaosema najinadi) lakini siwezi gawa hela bali nitatoa njia zilizonifanya nikafanikiwa mpaka sasa,itoshe tu kusema nilikua na moyo wa UDHUBUTU na nikaweza sasa ninaamini hata weweutaweza.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU BARIKI VIJANA WA TANZANIA