MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,104
- 6,827
Tom Mako: Kijana wa Kimaasai afunga ndoa na wanawake wawili wakati mmoja Kenya
Tom Mako, maarufu kama Junior, 27, alifanya sherehe hiyo ya harusi Jumanne wiki hii.
Mako anatokea kwenye familia ambayo ndo za wake wengi ama mitala ni jambo la kawaida.
Hata hivyo kuoa wake wawili kwa mpigo ni jambo amabalo halikuwahi kusikika katika jamii ya Kimasai ambayo wanandoa hao wametokea.
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Katika harusi hiyo ambayo ilipambwa vilivyo katika kitongoji cha Kisaju, Mako aliwaoa Elizabeth Silamoi, 24, na Joyce Tikoyian, 23.
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Mako alikutana na Bi Silamoi miaka miwili iliyopita wakati akichunga ng'ombe zake karibu na nyumabni kwa mwananmke
Mwaka jana akakutana na Bi Tikoyian pia akiwa anachunga ng'ombe karibu na kwao.
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Tikoyian amesoma mpaka kidato cha nne na Silamoi aliishia kidato cha tatu.
Katika mila za Kimasai, mahari ya ng'ombe hutolewa kabla ya kufungwa kwa ndoa, na bwana harusi Mako alikamilisha hilo ipasavyo.
Mako aliwaoa wakeze kimila japo wote walivalia mavazi ya kimagharibi. Mako alivalia suti ya rangi ya samawati na wakeze wakivaa mashela meupe. Wote pia walivalia urembo wa Kimasai.
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
"Nataka kuliweka sawa hili, harusi yangu ilikuwa ya kimila na haikuwa na mahusiano yoyote na kanisa. Kuna watu wanatuma habari za kupotosha mitandaoni kuwa ndoa yangu ilisimamiwa na wachungaji," Mako amenukuliwa na gazeti la Star la nchini Kenya
Amesema amewaoa wanawake hao kwa sababu wote wanampenda na hakutaka kumsononesha yeyote kati yao.
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
"Huu ni ujumbe ninaoutuma kwa waume wa kisasa wanaojifanya kuwa wanampenda mwanamke mmoja na huku wakiwalaghai kwa kuingia kwenye mahusiano na wengine pembeni," amesema na kuongeza:"Nimekuwa muaminifu kwa wake zangu kwa sababu sitakuwa na sababu ya kuongeza mke mwengine. Ninaamini wawili watanitosheleza."
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Bi Silamoi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye penzi na Mako, na kusema kabla ya kuja kwa mwenzake wawili hao walijadiliana kwa kina na kukubali
"Ninampenda. Nilimpa Baraka zangu kuongeza mpenzi. Nampenda (mke mwenzake) pia."
Bi Tikoyian, amesama wote wamekubaliana kuwa katika mahusiano ya aina hiyo na wazazi wake walikubali hilo kwa sababu wanamuamini Mako.
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Wazazi wa bwana harusi,Bw Mako Busabus na Bi Sintiyio, wamesema hawakuamini mwanzoni mtoto wao alipowaambia anataka kuoa wake wawili kwa siku moja, na sherehe moja. Lakini hilo lime
"Kwa umri wangu wa miaka 90 sijawahi kuona kitu kama hiki huku umasaini. Kwa kawaida, mtu anayetaka kuongeza mke husubiri kwanza walau baada ya mwaka au miaka miwili toka alipofunga ndoa ya kwanza," amesema Busabus.
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Mamorani wengine pamoja na wageni waliohudhuria harusi hiyo wanamchukulia Mkako kama shujaa kwa kufanya jambo ambalo halikuwahi kufanyika kabla umasaini.
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Haki miliki ya pichaHISANI/KINYANJUI
Baada ya harusi, watatu hao wamekuwa wakiendelea na maisha yao.
Haki miliki ya pichaPETER NJOROGE/BBCImage captionHapa wanaonekana wakiwa myumbani kwao Alhamisi
Haki miliki ya pichaPETER NJOROGE/BBCImage captionWakiwa nyumbani kwao