SI KWELI Kijana wa miaka 13 ameajiriwa na Google kutokana na uwezo wake

SI KWELI Kijana wa miaka 13 ameajiriwa na Google kutokana na uwezo wake

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
JC_TANMAY_22JAN_25 (1).jpg

 
Tunachokijua
Tanmay Bakhi ni mtaalamu wa teknolojia na mtengeneza programu tumishi, mwandishi, lakini pia ni mkufunzi. Tanmay ana chaneli yake ya youtube yenye zaidi ya wafuasi laki tatu pamoja na video zaidi ya 200 zikibeba mafunzo mbalimbali ya teknolojia.

Madai

Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambaa kikimuonesha kijana akifanya mahojiano huku ikidaiwa kuwa Kijana huyo wa kihindi Tanmay Bakshi (13) anayeingia darasa la tisa ameajiriwa na google nchini Marekani kwa mshahara wa Rs (Indian Rupee) 66 Lakh kwa mwezi. Taarifa hizi zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali Januari, 2025. Tazama hapa na hapa.

Uhalisia wa madai hayo upoje?

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli, Tanmay hajaajiriwa na google. Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia google reverse image search tumebaini kuwa video hiyo imekuwepo tangu mwaka 2017 tazama hapa na hapa huku nyingi zikiwa na madai yale yale kuwa kijana huyo ameajiriwa na Google.

Katika mtandao wa Facebook mwaka 2017 mtu mmoja alichapisha kipande hiko cha video na kuandika kuwa; “This kid is the smartest guest The AM Show has ever had, and he's only 13!”. Akiwa na maana kuwa "Mtoto huyu ndiye mgeni mwerevu zaidi katika kipindi cha AM Show, na ana umri wa miaka 13 pekee!"

Katika kipande hiko cha video kinamuonesha kijana huyo akijibu maswali mbalimbali aliyokuwa akiulizwa katika mahojiano kwenye show hiyo, ambapo mbali na mambo mengine alizungumzia kuhusu teknolojia ya Akili Mnemba (AI) umuhimu wake pia ameeleza kuwa anatoa mafunzo kuhusu teknolojia na kompyuta kupitia chaneli yake ya youtube na hakuna mahali alipozungumzia kuwa anafanya kazi Google katika mahojiano hayo.

Tanmay Bakshi kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) baada ya kusambaa kwa video yake mwaka 2017 zikiwa na madai kuwa anafanya kazi google alikanusha madai hayo tarehe 02/09/2017 kwa kwa kuandika kuwa; "For those who think I’m working with GOOGLE or facebook, I’m not - although I’d love to 🙂". Akiwa na maana kuwa “Kwa woe wanaodhani kuwa nafanya kazi na google au facebook, hapana sifanyi nao kazi ingawa ninatamani".
Back
Top Bottom