Kijana wa Miaka 19 ajitosa kugombea Urais nchini Uganda

Kijana wa Miaka 19 ajitosa kugombea Urais nchini Uganda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Miezi kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu wa Uganda utakaofanyika mwaka 2021, kijana mwenye umri wa miaka 19 amejitokeza na kuchukua fomu ya kugombea ofisi hiyo ya juu nchini humo.

Hillary Kaweesa amesema kuwa amewahi kuwa kiongozi na hivyo anakidhi vigeo vyabkuongoza nchi. Kukidhi vigezo atalazimika kuwa na milioni 20 za Uganda kama ada ya uteuzi.

Pia atatakiwa kukusanya saini 100 za wadhamini katika kila wilaya ambapo taifa hilo lina zaidi ya wilaya 100. Katiba ya nchi hiyo inaruhusu rai mwenye umri zaidi ya miaka 18 kugombea Urais.

Wengine watakaochuana kwenye nafasi hiyo ni Mbunge, Bobi Wine, Henry Tumukunde na Rais Yoweri Museveni ambaye atatetea nafasi yake.

1597389792024.png
 
Daaah 😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣

Kuishi kwingi kuona mengi. RIP mtunduizi Shaaban Robert, aaamin.
 
Katiba yetu umri wa kula bata,haitaki ugombee.Dogo akipita si atamuweka demu wake waziri mkuu
 
Back
Top Bottom