Kijana mwenye umri wa miaka 28, Ally Ngualo, mkazi wa Naipanga katika Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Nachingwea katika uchaguzi mkuu ujao.
Ngualo alisema kuwa sasa ni wakati muafaka kwa vijana kujitokeza na kuchukua nafasi za uongozi ili kuwatumikia wananchi na kuharakisha maendeleo katika maeneo yao.