Kijiji cha Emboreeti wilayani Simanjiro kifanywe sehemu ya kivutio cha utalii ili kuzalisha mapato

Kijiji cha Emboreeti wilayani Simanjiro kifanywe sehemu ya kivutio cha utalii ili kuzalisha mapato

Kijiji cha Emboreeti an utalii itawezekana!?

  • Naunga mkono hoja

    Votes: 2 50.0%
  • Kuwepo na mkakati

    Votes: 1 25.0%
  • serikali iunde tume

    Votes: 0 0.0%
  • wanakijiji wapewe elimu

    Votes: 1 25.0%

  • Total voters
    4

Mouse3

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
1,441
Reaction score
1,282
Wizara ya maliasili na utalii! Nimekuona bungeni Mheshimiwa naibu waziri ukijibu maswali kwa hisia nzuri ya kuendelea kuhifadhi mazingira na corridors na mazalia ya wanyama pori!

Kuna hiki kijiji kinaitwa Emboreeti wilayani Simanjiro! Ni eneo muhimu sana kwa mazalia ya wanyama pori hususani kwa hifadhi ya Tarangire, kabila la wazawa eneo lile wa Maasai ni wafugaji, ila nao sasa wanalima haswa, muingiliano wa makabila umekuwa mkubwa sio neno ni undugu na umoja wa kila mtanzania!

Ila sasa, huu ukataji wa miti, upanuzu wa mashamba kila kona kwakweli kunavuruga mfumo wa hawa wanyama pori, sichukizwi na kilimo ila uharibifu wa mali asili na kuheshimu mfumo wa hawa wanyama pori ambao kimsingi wamekutwa mule basi kuwepo na uangalizi angalau kwenye corrido zao za kuhama na mazalia yao!

Ni vurugu wakati wa kilimo watu wanafukuzana na wanyama usiku na mchana!

Ningeshauri pia kijiji hiki kifanyiwe utafiti kuwa sehemu ya kuipatia Serikali mapato kwa njia ya vivutio vya utalii na ikiwezekana kuwepo na geti la kuingilia Tarangire kwa upande ule, kwani itachochea uwekezaji wa mahoteli ya kitalii na kuamsha utalii wa cultural na mengineyo maana kijiji kina sifa zoote na materials yakuwezesha haya.

Na hili litapunguza wazo moja la kilimo tu na baadhi ya wananchi watahamia kwenye utalii na kutunza mazingira.

Wimbi la raia linalomiminika eneo hili mpakani na hifadhi ni kubwa, tahadhari isipochukuliwa soon Wizara mtaanza kutatua yale ya Ngorongoro.

Ni mtazamo tu!
 
Great MKUU na miondo mbinu nimeona imeboreka sana Barabara na Umeme Kituo cha Afyaa kijiji cha Nafco
 
Great MKUU na miondo mbinu nimeona imeboreka sana Barabara na Umeme Kituo cha Afyaa kijiji cha Nafco
Ile njia ina fursa za utalii lukuki! Nadhani serikali itupie jicho kule!
 
Back
Top Bottom