KWELI Kijiji cha Monowi nchini Marekani kina mkazi mmoja ambaye pia hulipa kodi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Je ni kweli Kijiji cha Monowi huko Marekani kina mkazi mmoja?

 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa BBC travel wanaeleza kuwa Monowi ni mojawapo ya miji mitatu iliyojumuishwa katika Kaunti ya Boyd, Nebraska ambayo ina wakazi wasiozidi 10. Monowi kwa sasa ina mkazi mmoja tu ajulikanaye kwa jina la Elsie Eiler. Miaka ya 1930 Monowi yalikuwa ni makazi ya watu 150 wakiwa na mgahawa, gereza, maduka na kanisa.

Maisha yalianza kubadilika Monowi mathalani ibada ya mwisho ya mazishi kufanyika Monowi ilikuwa ni mwaka 1960 ambayo ilimuhusu baba yake Elsie, kisha maduka na ofisi ya posta vilifungwa kati ya mwaka 1967 na 1970 kisha kufuatiwa na shule iliyofungwa 1974. Eiler ana watoto wawili, wajukuu watano na vitukuu wawili ambao wanaishi maeneo mengi.

Tovuti ya Eater walieleza kuwa Watu walianza kupungua Monowi na kuhamia maeneo mengine hadi kubakia wawili yani Elsie Eiler na Mumewe Rudy, hali ilibadilika tena mara baada ya Eiler kufiwa na mumewe mwaka 2004 na Monowi kubakiwa na mtu mmoja tu. Eiler amekuwa akiendelea kufungua baa yake iliyopo kwenye mji huo aliyoianzisha yeye na mumewe 1971 kabla hajafariki, hufungua baa hiyo kila jumanne hadi jumapili kuanzia saa tatu asubuhi.

Alipokuwa akihojiwa na BBC Eiler alisema β€œNinapoomba leseni za vileo na tumbaku jimboni kila mwaka wanazipeleka kwa katibu wa kijiji ambaye ni mimi, Kwa hivyo, ninazipata kama katibu, nizisaini kama karani na nimpe mimi kama mmiliki wa baa."

Eiler anasema miongoni mwa maswali ambayo amekuwa akiulizwa mara nyingi ni kuwa huwa hajihisi mpweke ambapo alijibu kuwa huwa anatembelewa na watu tofautitofauti mara kwa mara ambao jioni huondoka, wageni hao kila wanapofika Monowi husaini kwenye kitabu cha mahudhurio ili kutunza kumbukumbu.
SErikali ya Mama Samia inatakiwa kumsaidia huyo mwanakijiji.
Itamsaidia kivipi? Mbona hapo kwenye hicho kijiji si umeona kuna barabara ya lami? Ni kijiji gani hapa bongo kina barabara ya lami?
 
Mkuu tatizo kithungu,ile interview pale ubalozini nitaongea lugha ipi bila kujeruhi ulimi
Usishangae tuu- hebu litazame hilo kwa undani halafu uone kama linaweza kuwa ni fursa kwako.
 
Mkuu tatizo kithungu,ile interview pale ubalozini nitaongea lugha ipi bila kujeruhi ulimi
Usipate shida. Ubalozini utaongea Intanesheno (Ishara) au unaweza kumtumia mkalimani. Vyote vinakubalika.
 
Itamsaidia kivipi? Mbona hapo kwenye hicho kijiji si umeona kuna barabara ya lami? Ni kijiji gani hapa bongo kina barabara ya lami?
Kijiji cha Machame kina lami hadi chooni. KARIBU KILIMANJARO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…