OR TAMISEMI
Ministry
- Jul 3, 2024
- 20
- 93
Wananchi 3,149 wa kijiji cha Mundindi kilichopo Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wametengeneza historia ya kipekee baada ya Serikali ya kijiji hicho kuwakatia bima ya afya wanakijiji wote ili waweze kupata huduma ya afya bila kikwazo cha fedha.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kulipa fidia Shilingi bilioni 15 ili kupisha miradi ya Liganga na Mchuchuma ambapo kijiji hicho kilikuwa na eneo katika eneo la mradi huo na kukiwezesha kupata fidia ya Shilingi 464 milioni.
Kati ya fedha hizo, Sh400 milioni kijiji kiliamua kununua hati fungani katika moja ya taasisi ya kifedha hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo Julai 12, 2024 na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mundindi, Sapi Mlelwa wakati wa hafla ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya wananchi hao, iliyofanyika kijijini hapo