Kijijini wananiita Daktari

Daktari wa Meno

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2019
Posts
509
Reaction score
1,610
Baada ya kuzuka kwa gonjwa la Corona tuliletewa vikinga pua na mdomo (barakoa) na gloves za kuvaa mikononi hivyo vitu alitutumia mjomba mimi na mama na ndugu wengine.

Mama yeye anasema akivaa barakoa hapumui vizuri na wengine pia wanasema hivyohivyo ila mimi nimevaa naona kawaida na sema kweli nimependeza sana. Hadi sasa vijana wa kijijini wananiita Daktari maana nimevaa na shati refu jeupe.

Asubuhi navaa gloves na barakoa pamoja na shati langu jeupe refu naenda senta naongea nao yaani kama daktari na wengine wanajua kuwa naweza kutibu kumbe bado sijajua.

Sasa ni wiki imepita kila mtu anaiita daktari, daktari yaani ni raha kwa kweli na nimeomba wanitumie miwani yenye uzi wa kuning'inia ili wajue kabisa ni daktari.

Leo asubuhi walikuwa waniuliza mambo mengi sana hapa kijijini yanayohusu Corona nimewajibu vyema kabisa. Napendwa sana na wananchi yaani kila kitu kigeni huwa nawaonesha mimi pale kijijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…