Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
Unywaji wa KAHAWA hauleweshi na kuiondoa AKILI NA UTAMBUZI WA MWANADAMU.....
Unaweza kwenda kijiweni ukiwa na shilingi yako 100 kwa lengo la kupata KIKOMBE KIMOJA TU ilihali nafsi yako inataka kunywa VINGI....
Kama MWENYEZI MUNGU amekupa UCHESHI NA ULIMI FASWAHA WA KUNENA basi anzisha MADA inayovuta HISIA ZA WATU na uone kama hutasogezewa KICHUPA* ama FANTOM* 🤣🤣
1)KICHUPA
Ni chupa ndogo ya kuhifadhia vinywaji vya Moto ambayo huuzwa shilingi 500.Ndani yake huweza kuingia vikombe vya kahawa(vile vidogo) hata 12.
Sasa kumbuka umekwenda na shilingi 100 tu na "mdomo wako" ukakupa KICHUPA KIZIMAAA🤣🤣🤣
2)PHANTOM
Ni chupa kubwa(ya Kati) ambayo huweza kuingia hata vikombe vidogo 25 vya kahawa na huwa inanywewa kwa kushirikiana na wengine ila BINAFSI huwa ninaweza kuinywa peke yangu haswa STORI zikiwa zimenoga!!🤣🤣
SIGARA huuzwa kijiweni huko na vijiwe vingi hakuna masharti ya KUJITENGA PEMBENI ukitaka kuvuta SIGARA....Sigara huvutwa HAPOHAPO kuhanikiza STAREHE YA UTULIVU WA KAHAWA ikiwa inasambaa mwilini 🤣🤣
Ikiwa mnywaji wa KAHAWA havuti SIGARA ama ana mzio(allergy) na HARUFU PAMOJA NA MOSHI WA SIGARA basi atabaki kuwa "mnyonge" wa kushindwa kulalamikia HALI HIYO YA KUSAMBAZWA KWA MOSHI maeneo hayo 🤣🤣🤣
VIJIWE VYA KAHAWA hukaa watu wa kada na kaliba TOFAUTI ,kuna WASOMI was kiwango cha UDAKTARI hadi UPROFESA🤣🤣🤣
TUENDELEE KUBURUDIKA NA KINYWAJI CHETU PENDWA CHA KAHAWA!!!
#MnywajiKahawaVijiweMbalimbali
#AmaniUrafikiNaUpendoWaWatanzania
#KAZIIENDELEE
#TANZANIAKWANZA