Kijue kisiwa cha Ukerewe kwa undani. Kisiwa cha kifahari kilichopo pembezoni mwa jiji la Mwanza

Kisiwa hiki kinapatikana ndani ya Ziwa Viktoria nje kidogo ya jiji la Mwanza ambacho kwa ujumla wake kinaundwa na visiwa vidogo dogo vipatavyo 38 huku kisiwa kikubwa kikiwa ni kisiwa cha Ukara huku vingine vikiwa havikaliwi na watu.


Visiwa 38 havikaliwi na watu???--- kwanini wasiuze hiyo ardhi kwa watu binafsi kwa ajili ya kuwekeza???
 
Hapo kwenye nauli ya Basi,,mabasi yanapita wapi kuingia nansio,au Yana muundo wa hovercraft?

Pili,kisiwani Cha Kome kilichoungua juzi nacho kipo ukerewe au bukoba?
Kisiwa cha kome kipo Buchosa, unapita sengerema hadi Nyakalilo unapata zako kivuko cha Mv kome safi kabisa
 
Bado imani zipo hasa kule pande za Rubya na Lukara

Zinaweza kuwa zimepungua sana ila hazijaisha. Bado watu hawawezi kuua chatu maeneo ya Rubya hata akiingia ndani

Bado watu wanaamini kwenye kutumiana mamba.

Labda utufafanulie, ni kwanini kila anayeua chatu huko Rubya lazima apate madhara? Nilikuwa huko juzi juzi mwezi Machi, hizo Imani bado zipo
 
Ila mleta uzi ame generalise Sana,,hasa fursa,,je nijitaka kununua samaki wa biashara nakuja Hapo nansio?,
Dagaa je?.
Hebu nenda kiundani ili wawekezaji tuje kisiwani kuwekeza
Siyo simple kihivyo. Ngoja tusubiri jibu ila samaki nansio! Labda wa mboga tu
 
naskiaga wakelewe wengi ni black butterflies unazungumziaje hili?
 
Hahaa aya mkaruka chilimo karibhu ,, anye ndi bwiro kumulambo
Daah huyu bhana kanikumbusha sana sana home hongera hongera sana mleta maada leo nimejisikia amani na furaha kusoma uzi wa nyumbani thanks mr
 
Visiwa 38 havikaliwi na watu???--- kwanini wasiuze hiyo ardhi kwa watu binafsi kwa ajili ya kuwekeza???
Sidhani kama kaandika hivyo. Vipo ambavyo havikaliwi na watu ila vipo vinavyokaliwa na watu. Uwekezaji wa visiwani umeangalia sana uvuvi. Hivyo katika uwekezaji kuna sifa ya kisiwa lasivyo unaweza pata hasara kati ya maandalizi ya uwekezaji ukilinganisha na uzalishaji
 
Ninavyojua mimi wakala, wajita na wakelewe ni watu wenye kushabihana tabia na tamaduni kwa mujibu wa makabila yao.
Sasa kinachowarudisha nyuma kimaendeleo ni ile kasumba ya "wivu na chuki" dhidi ya waliofanikiwa, kasumba hiyo wamekuwa wakifanyiana sana wao kwa wao; yaani ndugu wa wanafamilia hataki nduguye afanikiwe kimaisha (hususani maendeleo ya kielimu).
Si ajabu Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita na kufanikiwa kwenda chuo akarogwa na mmojawapo wa wanaukoo. Ndiyo sababu wanafunzi wengi wakifaulu aidha kwenda kidato cha tano au kwenda chuo, huwa hawarudi vijijini kwao kipindi cha likizo.
Naliongea hili, kwa kuwa nilishashuhudia Mwanafunzi (kabila mjita) wa chuo cha Mzumbe tawi la Mbeya alifariki ktk mazingira ya kutatanisha mda mfupi baada ya kujiunga ktk chuo hicho.
 
Lazima siku moja nifike ukerewe my best destination
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…