Kijue kisiwa cha Ukerewe kwa undani. Kisiwa cha kifahari kilichopo pembezoni mwa jiji la Mwanza


hahahahahaaaaa, mkuu unaujasiri sana.
 
Mleta mada hapo kwenye imani za kishirikina bado panarudisha nyuma hicho kisiwa.mimi mzee wangu ni mkerewe alivyotoka mara ya mwisho kwenda shule Mzumbe hakurudi Tena mpaka kamuoa bimkubwa huku Kanda ya Kati tukazaliwa tukakua hajawahi kurudi ,Bibi mwenyewe na ndugu upande wa baba wao ndo walikua wanakuja.Mara ya Kwanza nimeenda Ukerewe tulienda kwenye mazishi ya Bibi Tena kwa kulazimisha
Mzee alikua hataki na tukapewa warning kibao mara usinywe maji,usipewe chakula na mtu usifanye hiki..dah Kuna wakerewe wanapaogopa kwao balaa.Baba zangu na mashangazi wote wapo mjini akirudi kwao ujue msiba na hawakai hata siku 3.huwa natamani Sana kujifunza kuongea kikerewe ila ndo hivyo Tena tunaongea lugha ya mama maana ndio ilotukuza.najua salamu to kikerewe.
 
Umejitaid kukipamba hiki kisiwa Mimi najua sifa hizi kwanza wauji sanaa kwa kutumia sumu ya mama, pili washirikina sanaa tatu wapo wengi usalama wa Taifa
 
Uko vizuri kwa taarifa Kama hizi,sema siku nyingine ingia ndani kwenye mambo ya mila na tamaduni zao nasikia mtu akifiwa na mme/mke huwa kuna taratibu fulani hivi zinafanyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii tunaita UTAKASO.. yani ukifiwa na mume lazima utakaswe na wazee hasa baba mkwe(baba wa mumeo)
 
Micind ni jina la kikelewe.. ila umeliweka kizungu, bibi yangu alikua anaitwa Msindi/ Mcindi
 
Hivi Igalla ndo kwa DPP Biswalo Mganga?
 
Nasikia huko kuoga hadharani sio ishu yaani...
 
Hujakosea mkuu, atakayepingana na wewe ni kwamba hayajui makabila hayo vizuri au ameamua kupotosha.
 

Umeandika ukweli mchungu mkuu!
 
Ukiwauliza wazee wanasema zamani watu wa kwenda au kutoka Ukerewe walitembea kwa mguu na hata wanyama kama tembo na wanyama wengine kutoka Serengeti waliweza kupatikana Ukerewe maana eneo lote linalofunikwa na maji kwa sasa kati ya Ukerewe na Kisolya inasemekana lilikuwa 'wetland' na mnamo mwaka 1917 Wajerumani walitengeneza channel badala ya kuzunguka Ukerewe kwa kwenda au kutoka Mkoa wa Mara ilikuwa rahisi kupitia hii channel, ambayo miaka ya 1960 walipojenga Bwawa la Owen na kunyesha kwa mvua kubwa inayojulikana Ukerewe kama 'Mvua ya Uhuru' kina cha maji ya ziwa kiliongezeka na kufunika eneo lote la wetland na kufanya Ukerewe kuwa kisiwa. Lakini inaonekana zamani mtu aliweza kutoka Ukerewe kwenda Kisolya au kutoka Kisolya kwenda Ukerewe kwa mguu. Hebu jaribuni kuuliza wazee unaowafahamu ili tuone kama wanaweza kusema hivi pia. Kuna details fulani niliziandika, nikizipata nitaongezea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…