Kijulikanacho kwa Icardi ndicho kilichofichwa kwa Naingollan

Kijulikanacho kwa Icardi ndicho kilichofichwa kwa Naingollan

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji alipoulizwa kuhusu kutomwita kiungo wa AS Roma, Radja Nainggolan kwenye kikosi chake akajibu kuwa ni kwa sababu za kiufundi mazima. Lakini wakati tunalijua sakata la Mauro Icardi basi yatupasa tujue na huku kinachoendelea.

Radja Nainggolan ni kiungo wa shoka ambae kiufundi ana fiti vema sana kwenye kikosi cha Roberto Martinez. Kitu kizuri ni kwamba Nainggolan anaweza kujipinda akacheza vema kokote pale kati kwaiyo kimfumo nampinga Martinez lakini kuna mahala naweza nikamwelewa yeye akiwa kama ni mtu mwenye mamlaka na wachezaji alionao kwenye kikosi.

Nainggolan ni mchezaji muasi. Ni mchezaji anaepinga vitu vingi wakati wachezaji wanaitwa kwenye timu ya taifa. Roberto Martinez wakati anajiunga na timu kwa mara ya kwanza aliweka wazi hataki mchezaji avute sigara wakati wa kambi lakini Nainggolan hakutii amri hii. Huyu alipewa chumba kizima ili aweze kuvuta sigara kila siku na kiufupi hakuna bosi ambae anakubali mfanyakazi awe juu yake.

Nainggolan alikasirika vibaya na kutukana na kupiga makelele sana hata mpaka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati anatolewa sub mechi na Italy kwenye michuano ile ya Euro ya mwaka juzi. Nainggolan alikamatwa na polisi akiwa amelewa wakati gari yake ikiwa imepata pancha lakini alichelewa mazoezi ya kiufundi huku Martinez akizumgumzia swala la nidhamu siku hiyo na kama haitoshi, Nainggolan alimuudhi sana Martinez baada ya kuonekana akicheza mechi ya kirafiki dhidi timu ya watoto huku akiondoka kwenye kambi ya timu ya taifa kwa sababu ya majeruhi na hii ilitokea miezi 3 baada ya Martinez kuchukua timu.

Kitu ambacho mashabiki wengi huwa hawakizungumzii ni nidhamu na vitu ambavyo vipo nje ya uwanja. Makocha huwa hawaogopi hata kufukuzwa kazi lakini hawako tayari kuona sikio likizidi kichwa na ni wazi hata bila ya kupepesa macho kwamba Martinez na Nainggolan haziivi. Hili sio swala binafsi tangu Martinez achukue timu limekuwa likimkera sana. Nainggolan hatii maelekezo yake. Kila anachoongea basi ni ama kinapingwa au hakifanywi vizuri na Martinez. Nainggolan ni "Rebellious figure" ndugu zangu anapokuwa timu ya taifa.

Mashabiki wanapaswa kulijua hili na ndio maana hata Wabelgiji wenyewe huwaoni wakilalamika chochote sana sana japo imewauma lakini alichofanya Martinez ni kulinda heshima ya timu. Makocha huwa wanaangalia vitu vingi kwa wachezaji wao zaidi tu ya vile ambavyo mashabiki wanavifurahia ndani ya uwanja.

Najua wapo walioumia lakini unapojua faida na maana ya nidhamu ndio unaweza kujua kwanini watoto wa kizungu huwa hawapigwi bali huwa wanapokonywa vile wavipendavyo. Kwa kocha kitu kikubwa anachoweza kukifanya ni kutomwita tu mchezaji. Martinez angeweza tu kumpiga faini Nainggolan kwa vitendo vyake lakini alijua kuwa atakapokosa kombe la dunia basi atajifunza somo. Ni maamuzi magumu kiukweli lakini mchezaji asiyetii amri za mwalimu ni sawa na mhalifu ambae anaevunja sheria.

Sema tu alichokosea Martinez ni kuudanganya umma lakini pengine angeweka wazi kama ukweli wa Icardi ujulikanavyo basi isingekuwa shida kubwa maana kwa wenzetu nidhamu ndio kila kitu haijalishi mchezaji ni muhimu kiasi gani kwenye timu na anategemewa vipi. Mimi binafsi najua uwezo na umuhimu wa Nainggolan lakini huwezi kuanza wala kujua jinsi ya kumlinda tu mchezaji asiyefuata amri za mwalimu bila ya kuangalia pia na upande wa pili.

Tatizo ni kwamba watu wameangalia upande mmoja peke yake lakini unapoweza kujivisha uhusika wa Martinez kama mwalimu basi unaweza kuelewa kwanini vitu vingine huwa vinafanyiwa maamuzi magumu. Kazi inaweza kupotea, mashabiki wakakutukana na kukuona mbaya lakini kila kazi inahitaji maadili na nidhamu. Mpira sio tu ndani ya uwanja bali tabia na mwonekano wa mchezaji nje ya uwanja pia.

Na moja kati ya vitu ambavyo vinafanya mpira wetu usiendelee ni kulea utovu wa nidhamu kwa sababu tu mchezaji fulani ni mzuri au anategemewa. Narudia alichokosea tu Martinez ni kusema kuwa kimfumo Nainggolan hamfai lakini hakuna shaka nidhamu ya Nainggolan ndio imemponza.

Sisi tumezoea kuona Kichuya akitolewa na kukataa kukaa benchi la ufundi akiweka headphone masikioni na mechi inayokuja akacheza tena kwa kuanza lakini tusikariri hivi pia na kwa wenzetu. Utovu wa nidhamu hauangalii uwezo wala kipaji, imewauma wengi Nainggolan kutoenda urusi lakini Je kocha asiamue kulingana na kile anachokiamini? tumsamehe tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duu ila naona tayar ametuhujumu wapenz wasoka hayo yanyuma yacapet hayatuhusu huyu mtukutu alikua burudan tosha, no naingollan, no balotel, no vidal, no ibra cadabra radha hakuna
 
Naingollan ni fundi, Kocha ameboronga kabisa kumuacha. na watamkumbuka
 
Nidhamu nidhamu nidhamu ndio iliyoizamisha Taifa Stars, timu ya taifa ya Tanzania.

Miaka ya nyuma kocha toka Brazil, Marcio Barcelio Maximo alivyoanza kuinoa Taifa Starz, haikupita muda mrefu akawashutumu akina Amir Maftah ambae alikuwa beki wa kushoto wa timu hiyo na Simba, Haruna Moshi, Juma Kaseja ambae watanzania wasio na akili walimbatiza jina la Tanzania 1.

Sababu kuu ya kuondoka kocha huyu ni kuitwa mbishi, jeuri na kichwa ngumu na vyombo vya habari vya Tanzania na mashabiki. Maximo kiuhalisia aliinua saaana soka la Tanzania na watanzania waliipenda mnoooo timu yao ya Taifa kuliko miaka ya hivi karibuni. Mpaka Maximo anaondoka bado alisimama ktk misimamo yake kama akina hao Martinez na Sampaoli wa Argentina. Ikafika kipindi mpaka vijana wa Taifa Starz wakawa hawamheshimu tena kocha wao, Marcio Maximo hivyo kukawa na matokeo mabovu na kocha kutimuliwa.

Kuanzia hapo timu ya Taifa sikuona teeena ikiinuka na kuwa ktk spirit nzuri kama kipindi kile, ile spirit ya miaka ile tungedumu nayo miaka hata 5 leo hii hii timu ingekuwa ni ya kuogopwa Afrika Mashariki na kati.
 
Naingollan ni fundi, Kocha ameboronga kabisa kumuacha. na watamkumbuka
yaaani pamoja na fact zote alizoziongea mtoa mada dhidi ya huyo mchezaji " lakini bado mnapinga kuhusu maamuzi ya coacher....aisee...kweli tz wabongo ni mzigo linapokuja suala la kufikiri
 
yaaani pamoja na fact zote alizoziongea mtoa mada dhidi ya huyo mchezaji " lakini bado mnapinga kuhusu maamuzi ya coacher....aisee...kweli tz wabongo ni mzigo linapokuja suala la kufikiri

Kwanza kocha hakuzungumzia popote kuhusu suala la nidhamu, alizungumza kuhusukuwa kuwa hafiti kwenye mfumo wake. na ndio jambo ambalo haliingii akili kabisa.

Na kama anamatatizo mbona Roma wanakwenda nae vizuri tu na hatuoni matatizo yoyote. Ukiwa kama kocha mkubwa lazima uwe na uwezo wakuhandle watu wa aina tofauti.
 
Kwa kipindi hicho KASEJA alikuwa Tz 1.
Labda mimi ndio sikuelewa.
Nidhamu nidhamu nidhamu ndio iliyoizamisha Taifa Stars, timu ya taifa ya Tanzania.

Miaka ya nyuma kocha toka Brazil, Marcio Barcelio Maximo alivyoanza kuinoa Taifa Starz, haikupita muda mrefu akawashutumu akina Amir Maftah ambae alikuwa beki wa kushoto wa timu hiyo na Simba, Haruna Moshi, Juma Kaseja ambae watanzania wasio na akili walimbatiza jina la Tanzania 1.

Sababu kuu ya kuondoka kocha huyu ni kuitwa mbishi, jeuri na kichwa ngumu na vyombo vya habari vya Tanzania na mashabiki. Maximo kiuhalisia aliinua saaana soka la Tanzania na watanzania waliipenda mnoooo timu yao ya Taifa kuliko miaka ya hivi karibuni. Mpaka Maximo anaondoka bado alisimama ktk misimamo yake kama akina hao Martinez na Sampaoli wa Argentina. Ikafika kipindi mpaka vijana wa Taifa Starz wakawa hawamheshimu tena kocha wao, Marcio Maximo hivyo kukawa na matokeo mabovu na kocha kutimuliwa.
 
Duu ila naona tayar ametuhujumu wapenz wasoka hayo yanyuma yacapet hayatuhusu huyu mtukutu alikua burudan tosha, no naingollan, no balotel, no vidal, no ibra cadabra radha hakuna
Kweli tutawamisi hao vichaa .. kuna burudani flan hv
 
Kwa kipindi hicho KASEJA alikuwa Tz 1.
Labda mimi ndio sikuelewa.
Ni kweli, LAKINI ile issue ya kuchukua mke/demu wa mchezaji mwenzake (simkumbuki ni nani) ikamfanya MAXIMO asimwite timu ya Taifa na badala yake akawa anamtumia IVO MAPUNDA.

Wenzetu issue ya nidhamu ni kipaumbele, angekuwa kocha mzawa angeogopa kumdrop Kaseja.
 
Kwanza kocha hakuzungumzia popote kuhusu suala la nidhamu, alizungumza kuhusukuwa kuwa hafiti kwenye mfumo wake. na ndio jambo ambalo haliingii akili kabisa.

Na kama anamatatizo mbona Roma wanakwenda nae vizuri tu na hatuoni matatizo yoyote. Ukiwa kama kocha mkubwa lazima uwe na uwezo wakuhandle watu wa aina tofauti.
kwani rijkard alivyokuwa anayofauti na ronaldinho " aliwahi kusema kuwa dinho anatoka na mwanae..." mambo mengine yanabaki " chini ya capert ndio maana ya taasisi...sio lazima kila kitu mpaka ufahamishwe...though taasisi yao wenyewe inatambua fika kuwa "" shida iko mahala gani "" .....Alex Ferguson alimpiga kiatu " becks...lakini hakuwa wahi kusema kuwa wanaugomvi wowote nihabari tu ambazo zilikuja kulick baada ya watu waliokuwepo changing room kusema hiyo siri.....na huwenda Martinez alifanya hivyo makusudi " ili wadau wa soccer wasipate nafasi ya kuwasulihisha
 
yaaani pamoja na fact zote alizoziongea mtoa mada dhidi ya huyo mchezaji " lakini bado mnapinga kuhusu maamuzi ya coacher....aisee...kweli tz wabongo ni mzigo linapokuja suala la kufikiri
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

SASA Mkuu mtu kama huyo huwa najiuliza kichwani mwao huwa wanamiliki juice au uji wa ulezi
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

SASA Mkuu mtu kama huyo huwa najiuliza kichwani mwao huwa wanamiliki juice au uji wa ulezi
Mtihani sana mkuu"" yaani mtu anashindwa kabisa kutambua kuwa utovu wa nidhamu ..unaweza kuwa sababu ya kuwatoa morali ya mapambano wachezaji wengine ....hajiulizi..kwanini basi john tery alivuliwa unahodha ..baada ya kufikwa na tuhuma ya kutembea na mke wa mchezaji mwenzake ... Goran Erickson kwanini aliacha kuendelea na kuifundisha uingereza baada ya kufikwa na tuhuma ya ngono "" .........yaani sijui tuna vijana wenye Mawazo ya namna gani "",..aiseee kama taifa ndio linategemea vijana kama huwa kuwa ndio nguvu ya taifa ....."" tusubiri kuona taifa likibakwa tu""
 
Mtihani sana mkuu"" yaani mtu anashindwa kabisa kutambua kuwa utovu wa nidhamu ..unaweza kuwa sababu ya kuwatoa morali ya mapambano wachezaji wengine ....hajiulizi..kwanini basi john tery alivuliwa unahodha ..baada ya kufikwa na tuhuma ya kutembea na mke wa mchezaji mwenzake ... Goran Erickson kwanini aliacha kuendelea na kuifundisha uingereza baada ya kufikwa na tuhuma ya ngono "" .........yaani sijui tuna vijana wenye Mawazo ya namna gani "",..aiseee kama taifa ndio linategemea vijana kama huwa kuwa ndio nguvu ya taifa ....."" tusubiri kubakwa tu
JOHN TERRY alikula dem wa WAYNE BRIGDE.
Akamtoa jamaa kwenye mood ya soka kabisa.
 
Ni kweli, LAKINI ile issue ya kuchukua mke/demu wa mchezaji mwenzake (simkumbuki ni nani) ikamfanya MAXIMO asimwite timu ya Taifa na badala yake akawa anamtumia IVO MAPUNDA.

Wenzetu issue ya nidhamu ni kipaumbele, angekuwa kocha mzawa angeogopa kumdrop Kaseja.
Kibongo bongo Hatuwezi..
 
JOHN TERRY alikula dem wa WAYNE BRIGDE.
Akamtoa jamaa kwenye mood ya soka kabisa.
hahaaaa una kumbuka eeehh"" Jamaa akawa hapokei hata mkono wake .....dahhhh "" kweli papuchi noma "" ila huo icard ndio kazidi aiseeee...kapitiliza
 
Kwanza kocha hakuzungumzia popote kuhusu suala la nidhamu, alizungumza kuhusukuwa kuwa hafiti kwenye mfumo wake. na ndio jambo ambalo haliingii akili kabisa.

Na kama anamatatizo mbona Roma wanakwenda nae vizuri tu na hatuoni matatizo yoyote. Ukiwa kama kocha mkubwa lazima uwe na uwezo wakuhandle watu wa aina tofauti.
Mourihno wachezaji wengi huwa hawafiti ktk mifumo yake lakini... wakienda sehemu zingine wana wika mf. Zeruzeru, Mo wengine utaongezea... hata kipindi cha babu pia wakina folan, veron, nk hawa kuwika ktk mifumo ya babu fergie lakini wali wika sehemu zingine...

bora huyu kocha kasema kweli kuliko kumuita na kuto mtumia, kama yahya toure yupo man city lakini hatumiki...
 
Back
Top Bottom